Wakuu naomba msaada na sitorudia tena

Kabaizer

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
504
Reaction score
64
Za asubuh jamani,mimi ni mvulana ambaye nina girlfrnd,tunapendana na kuaminiana na tumeshaduu kama mara 10 hivi.
Ila siku hiz za karibuni nilikua nikiduu naye sehem zangu za siri zinaniuma sana tena sanasana sehem ambayo mkojo unatokea na sasa hivi nipo home naenda chooni kukojoa kabla sijakojoa nimekuta kitu kama usaha katika tundu linalotoa mkojo.kwa kifupi naumwa ila sijui naumwa nini na nitumie dawa gani ili nipone,naomben msaada wenu jamani.
natanguliza shukrani.
 

ushauri nenda hospitali watachukua vipimo na utapatiwa dawa sahihi kulingana na tatizo lako usisahau kuambatana na mwenzi wako ili kumaliza tatizo. Angalizo pima na kipimo kikubwa ili uwe na amani zaidi
 
Nyie watoto kwanini mnavamia mambo ya wakubwa angali umri mdogo? Haya gono/kisonono hiyo....! Wahi hospitali na mpenzi wako wote mtatibiwa...!
 
Mkuu Kabaizer, Pole, bado tunashauri vijana kusubiri!

-Una umri gani?
-Je, maumivu yako hapo kwa muda gani?
-Maumivu yapo hapo kwa muda na ni ya namna gani?..kuna uelekeo wowote?..
-kuna dalili nyingine kama kuwashwa, kukojoa damu(kuona tone/matone ya damu), maumivu wakati wa kukojoa?

- Je mnapofanya tendo hilo mnatumia kinga?Mara zote?
- Je dalili girlfriend wako analalamika tatizo lolote au huko kabla?
 
hiyo ni U.T.I Usiogope sio gono
 
Reactions: awp
duuh asanteni wakuu,nikipona naleta certificate zangu
 
ngono bila kinga ni hatari hasa kisono ama kaswende,nenda kapime uli upate tiba mapema.
 
usijar bwana joseph haule utaletewa tu
 
umri miaka 22
maumivu yapo takriban wiki mbili
maumivu yanakua kwa muda kuna siku naamka nipo saf kabisa,ila toka juz hali imezid kua mbaya.
dalili za kuwashwa,kukojoa damu,tone au matone ya damu hakuna,ila maumivu wakati wa kukuojoa yapo.
huwa hatutumii kinga kabisa.
girlfrnd wangu halalamiki kitu ila wakati wa kusex huwa anatoka haruf flani hivi ambayo siielewi.
 

Ni vizuri wewe na mwenzio muwahi hospitali mkachekiwe na kupata matibabu nadhani mtakuwa na Sexual Transmitted Diseases S.T.D
 
unaposema hutarudia tena unakusudia nini?je! ikitokea ukirudia !.cha msingi wahi hospitali fasta ndio njia pekee ya kukusaidia kwa haraka na baada ya hapo acha kwenda peku kwa watu usiokuwa na uhakika nao.
 
Na yeye(dem wako) atakumbwa na hilo gonjwa siku si nying zijazo.... nendeni wote.. andaeni kama 100000 flani kwa tiba yenu wote... kuna tiba ya vidonge na sindano ya mshipa wa mkono... mtapona haraka zaidi.... niliuguz mdogo wangu alpopatwa dalili kama hizo..ila ye aliwahi kuniambia mapema...
 
Mko wangapi? Pelekeni hizo nini zenu kwa doctor haraka.
 
Wote wawili mtakuwa na gonorrhea. UTI haina dalili hizi. Msichana wako atakuwa hajui sababu dalili kwa wanawake ni tofauti na si Kali Kama kwa wanaume.
soma link Gonorrhea - PubMed Health

Cha muhimu nendeni wote hospitali. Tumia kinga wakati wote, na muulize mko wangapi. Pima na ukimwi kabisa. Ukitoka negative shukuru mungu. AIDS is very real!


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…