Wakuu naombeni msaada wenu tafadhali

kibol

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
4,521
Reaction score
2,747
Nimeanza kuugua tarahe 14/01/13,baada ya kusikia maumivu makali ya kichwa,mafua makali pamoja na kukohoa kwa hapa na pale,siku inafuatia nikaenda kupima malaria nikaambia iko 2,nikachukua dawa mseto nimemeza iyo dozi leo ndio ninamalizia,ila tatizo ni homa za mara kwa mara ambazo huwa ni kali sana,kuna wakati mchana nasikia baridi sana wakati mwili unajoti kali,imagine npo sinza huku nazima feni najifunika na bado natetemeka,hivyo hivyo na wakati wa usiku kuna muda homa inakua kali mno mpaka naona km hizi dawa hazinisaidii au labda kuna ugonjwa naumwa zaidi ya malaria,naomba nisaidiwe jamani nifanye nini?nikapime tena magonjwa mengine au?
 


Jibu ni hiyo au.
 
jaribu kuchek taifodi,kiasi cha damu pima na damu yenyewe kama inapungukiwa virutubisho muhimu ili ushauriwe aina ya vyakula na matunda na ikibidi cheki na HIV
 
Usiogope,homa kama yko imeniisha juz tu hapa,kunywa maji mengi pia kula machungwa utapona ndg yng.usisahau pain killers.
 
cha umuhmu n kuzngatia kunywa dawa kwa umakini. USIDHARAU PALE DR ANAPOKUPA PANADOL UMEZE, pia ukachek kama una typhord
 
jaribu kuchek taifodi,kiasi cha damu pima na damu yenyewe kama inapungukiwa virutubisho muhimu ili ushauriwe aina ya vyakula na matunda na ikibidi cheki na HIV

ndugu yangu LOOOK nashukuru sana kwa ushauri wako,ngoja niufanyie kazi
 
Last edited by a moderator:
Usiogope,homa kama yko imeniisha juz tu hapa,kunywa maji mengi pia kula machungwa utapona ndg yng.usisahau pain killers.

nadhani hapo kwenye machungwa umenigusa bro,ngoja niyatafute yakutosha cuz nakula mananasi tu ndugu yangu,nashukuri kwa kunijali,asante kwa ushauri
 
cha umuhmu n kuzngatia kunywa dawa kwa umakini. USIDHARAU PALE DR ANAPOKUPA PANADOL UMEZE, pia ukachek kama una typhord

mkuu Jonash well said na nimekuelewa,asante sana
 
Last edited by a moderator:
Hebu rejea kwanza historia ya mahusiano yako uangalie ni wangapi umewakwaa. Kama unawajua wote angalia hali zao na kama huwajui nenda kapime tu.
 
Mkuu kibol mimi ninakupa Dawa ya kutibu Malaria sugu uliyokuwa nayo tumia kisha unipe feedback:

Dawa ya kutibu Malaria.


Katakata Vitunguu saumu sawasawa. Meza kijiko kimoja cha vitunguu hivi mara tatu kwa

Siku na kunywa lita 2 za limao glasi ya chai kwa siku. Endelea na tiba hii kwa siku 5.
 

mkuu MziziMkavu nashukuru sana kwa dawa yako,nashukuru sana kwa kusacrifice muda wako bure nakusaidia wengine,mwenyezi Mungu akuzidishie maradufu pale unapopunguza kusaidia wahitaji.
 
Last edited by a moderator:

Get H.I.V test
 
Sidhani Kama una typhoid kwani typhoid haina dalili za Mafua nafikiri unaweza kuwa na viral infection, it might be influenza Mara nyingi maambulizi ya virus hayana tiba ni kuiachia tu kinga yako ya mwili ifanye kazi unachojitaji ni kula vizuri hasa matunda yenye vitamin c kwa wingi na kupumzika labda na pain killer kwa ajili ya maumivu Lakini ni vyema kupima vipimo vingine vya damu Ili kuondoa hotu ya maradhi mengine yenye dalili Kama hizo.
 

Mkuu, kutokana na kuibuka kwa dawa nyingi za malaria (za hospitali) imekua ngumu sana mtu kujua ni dawa ipi hasa inafanya kazi vizuri na haina madhara mengine ambatanishi. Nimeipenda hii, sidhani kama itakuwa na side effect.

Naomba ufafanuzi wa yafuatayo kuhusu hii dawa mkuu:-
- Hapo kwenye red sijakupata vizuri, lita 2 za limao glasi ya chai kwa siku. lita 2 za maji?
- Hii inaweza kutumika kama kinga au ni kwa ajili ya kutibu tu.

Nashukuru sana mkuu. Ubarikiwe
 

Pole sana ndugu yangu. Nilienda TMJ tar 12 - Jan nikiwa na homa kali, mwili unachemka na kusikia baridi, nikaambiwa na malaria, watu wengi niliowakuta pale walikua wanalalamika homa kali zinazoambatana na kifua na kikohozi, kusema kweli sijajua ni kitu gani kimesababisha hali hii kuanzia Dicembar hadi sasa kwa watu wengi (wataalam watusaidie).

Kapime tena kama malaria imepona vizuri, kunywa maji mengi kama wadau walivyoshauri na upate muda wa kupumzika mkuu.
 
Mkuu Samaritan ukisha tumia hiyo inakutibu na kuuwa wadudu wa ugonjwa wa malaria unakuwa huna tena Malaria.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…