kibol
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 4,521
- 2,747
Nimeanza kuugua tarahe 14/01/13,baada ya kusikia maumivu makali ya kichwa,mafua makali pamoja na kukohoa kwa hapa na pale,siku inafuatia nikaenda kupima malaria nikaambia iko 2,nikachukua dawa mseto nimemeza iyo dozi leo ndio ninamalizia,ila tatizo ni homa za mara kwa mara ambazo huwa ni kali sana,kuna wakati mchana nasikia baridi sana wakati mwili unajoti kali,imagine npo sinza huku nazima feni najifunika na bado natetemeka,hivyo hivyo na wakati wa usiku kuna muda homa inakua kali mno mpaka naona km hizi dawa hazinisaidii au labda kuna ugonjwa naumwa zaidi ya malaria,naomba nisaidiwe jamani nifanye nini?nikapime tena magonjwa mengine au?