Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Wakuu amani iwe kwenu,
Naenda kwenye mada moja kwa Moja,
Wiki Moja kabla ya Xmass nikiwa Nimetuna sehemu karibu kabisa na home napiga zangu masanga, mara ghafla kaja dada yangu, akaniambia fulani anakuita (jina kapuni) basi bwana dakika sifuri nikafika nilipoitwa basi ikawa hivi:
Ooh Samahani Bushmamy, nikamwambia usijali, akaendelea tena. Samahani nina mgonjwa wangu naomba umuhifadhi kwenye kibanda chako cha nje kwa siku 4 tu, nikamwambia haina noma mbona, mwambie basi dada atengeneze mazingira waingie, mimi nikasepa zangu kwenye mishe zangu.
Kutokana na kuwa busy na mambo yangu sijawahi uliza huyo mgonjwa anaumwa nini maana na wala sikujua ni nani ila Nilijua ni wanawake maana niliwaona, Basi bwana mwaka mpya nkaamua kutulizana home na kupikia machalii wangu siku hiyo.
Basi bwana maandalizi siku hiyo nayafanyia nje maana nilikuwa napikia Mkaa, huyo mama mmoja (wote ni wamasai) akaniambia Bushmamy nataka pilau na mimi nikamwambia usijali. Basi wakati niliendelea na shughuli zangu pale nje ndo nikawa namuuliza vipi kokoo (bibi kwa kimasai) anaumwa nini akasema ni kifua maana alikuwa akikohoa sana usiku. Na Mchana kumbe anaumwa asthma sijui ndiyo pumu? Siku ikaishia.
Baada ya siku mbili tatu nipo kwenye Mishe zangu nikasema acha niende home mara moja kuna kitu nilisahau. Dah kufika tu hivi nipo nje Nasikia mtu anahema vibaya sana nikakimbia haraka kule waliko wamasai. Dah nacheki hivi ni yule Kokoo kuzidiwa kifua kimembana haswaa kuongea hawezi na jasho linamtoka mbaya kabisa huku mate yanamtoka nikakimbia mbio kwenda kumuita huyo mama anaemtibu kumbe naye huyupo, Basi mwanae mmoja hapo akaja akamuona masai na ile hali anaogopa sana na yeye akaongea nao kimasai. Huku ananielezea maana hawajui Kiswahili wanajua kidogo sana.
Ile hali iliendelea vile kwa muda huku tukiwa hatujui tufanye nini, baada ya muda hali ile ikapungua nikasepa zangu,
Sasa usiku wa saa kumi nikiwa nimelala ndani nikasikia mtu anagugumia kwa sauti kubwa nikasikilizia basi nikajua ni yule mgonjwa, nikampigia simu yule anaemtibu (nyumba zinaangaliana) kuwa mgonjwa wake hayupo fresh basi akawa amekuja anaongea nao kimasai. Mi wala sikutoka ila naona alimpa dawa (anamtibu kwa kutumia mitishamba)
Asubuhi nikaondoka zangu muda huo nikawa nipo mtaa wa pili. Nkapitia dukani kwa mama mmoja wa Kiarusha sasa wakati nipo pale yule mama wa kimasai anaemuuguza mwenzake akawa amekuja pale nikamuuliza vipi mgonjwa? Sasa vile lugha hatuelewani yule mama pale dukani akawa anitafsiria, sasa maelezo yenyewe ni kama hivi
Huyo bibi mgonjwa tangu amekuja kutibiwa hapo kwenye mitishamba hamna nafuu yoyote. Ile bali hali ya mgonjwa ni ile ile na bado inazidi kuwa mbaya, huko kwao walikotoka tayari kijana wake na huyo mama mgonjwa ameshauza ng'ombe watatu na kuleta hela hapa kwa huyu mama anaemtibu japo hamna nafuu yoyote,
Pia jana kijana wake kapigiwa simu kuwa inatakiwa kesho alete laki na nusu kwa ajili ya kuendeleza dozi kwa hiyo kijana anauza ng'ombe nyingine ili alete hela kesho kwa huyu mama.
Huyu mama anaendelea kusema kuwa alikutana na binti yake na huyu mama anaetoa dawa Hospitalini ndo akawaambia kuwa mama yake anatibu vizuri sana kwa miti shamba na watu wote wanaoenda kwake huwa wanapona basi ndo wakatoroka Hospital na kuja kutibiwa hapa
Sasa baada ya kuona hamna unafuu wowote wakitaka kuondoka ili waende Hospital huyu mama anaemtibu pamoja na mgonjwa wake wanakataa, lakini huyu anaemuuguza pamoja na kijana wa mama mgonjwa wanataka wamrudishe Hospital lakini mgonjwa nae anakataa sasa wanahisi labda huyu mama kuna jambo kamfanyia huyo mgonjwa ili aendelee kula hela zao.
Sasa na mimi naogopa kwa kweli maana hata msichana wangu hapa anasema juzi kuamkia jana kuwa mgonjwa alikuwa anagugumia kwa sauti kubwa sana hadi yeye akaogopa.