Wakuu, ni kwa nini kizazi hiki cha sasa kinaona ugumu kutumia herufi H kiusahihi?

Cliffhanger

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2018
Posts
721
Reaction score
1,293
Wakuu, ni kwa nini kizazi hiki cha sasa kinaona ugumu kutumia herufi H kiusahihi? Neno Habari linaandikwa Abari, Hujambo inaandikwa Ujambo, Hayupo inaandikwa Ayupo. Mengine mtaongezea.

Mwanzoni nilifikiri kuwa ni uvivu wa kuandika maneno mengi, kilichonishangaza ni kuwa hata sehemu ambayo inatakiwa itumike A tupu panaandikwa Ha, Kwa mfano neno Amekubali linaandikwa Hamekubali.

Je tufanyeje kama wana Jamii kurekebisha tatizo hil?
 
Ukweli ni kwamba vyakula laini vinaharibu sana vijana wetu
Hasahasa chips
Unakuja kijana anamindevu lakini anaogea utadhani bint
Hasahasa wanaume wa dar
 
Watu wameathiriwa na MOTHER TONG zao
 
haha, wewe jamaa una yako ya ziada!
 
Suluhisho ni kukanyaga fimbo wote wenye uandishi huo.
 
Hahaja hanasema akukute pale sipendi kwa kweli kuna wale wa L na R kuna wale xx kuna wale wa k,p, hua nachoka kabisa kuendelea kujib sms za hivi
 
Watu wameathiriwa na MOTHER TONG zao
Mmmh,,sidhani. Mi Nina watu nimesoma nao mjini hapa darasa LA kwanza mpaka LA saba,,siku hzi gafla anaandika ivo,,,nahisi wanadhani ni fasheni wakati ni ushamba tu.. Ingawa wahaya na watu wa musoma ndo wanashida iyo
 
Ukweli ni kwamba vyakula laini vinaharibu sana vijana wetu
Hasahasa chips
Unakuja kijana anamindevu lakini anaogea utadhani bint
Hasahasa wanaume wa dar
Hata Insta live huijui bado. . . . We ni jini kisirani!!
 
Haipendezi kwa kweli,inabidi wajifunze kuandika kiufasaha
Nalog off
 
Mimi hua najiuliza,hivi na huko mashuleni mwao hua wanaandika hivyo? mtu anaandika "Alafu" badala ya "Halafu"
 
Back
Top Bottom