Wakuu nifanyeje nilijue draft?

Najipa big up maana huwa naweka level ya 100 kwa Dalmax checkers namkalisha mi binafasi kwa sasa nipo level ya juu sana,
Nilianza kucheza draft nna miaka 10.

Dalmax level yake ni moderate, unaweza kumfunga lakini ukawa kiwango cha kawaida tu.
 
Hahahaahahaaa kwanza darasani somo la hesabu ulikuwa unapataje???

Amini nakuambia mabingwa wote wa draft wanajua hesabu hata km hawakwenda shule.Draft ni mchezo wa Akili na wenye uwezo mkubwa wa kufikiri ndo wanashinda otherwise utakuwa mchezaji wa Copy flani na ikipanguliwa kdg unafungwa vby sana
 
Kaka mimi nimeshawahi kuiwakilisha Tz kwenye michezo ya jumuia ya Madola kwa mchezo wa draft, usinichukulie poa

Nakukubali mwanangu, maana uliwahi kunipa changamoto kipindi kile kwenye ile ligi yetu na wa ukae bin kulijua.
 
acha ujinga drafti hata urirudierudie mara nyingi na hata kama wewe ni mhandisi au mwana mahesabu vipi usipokuwa na kipaji na drafti huwezi kuwa mjuzi nalo. we fikiria waliokimbia shule, au watu wa kawida kabisa ambao hawajui hata kusoma wanalijua drafti kuliko wewe unaejua hesabu. ko draft ni kipaji tu! kama ulivyo mpira na michezo mingine!! kila mtu ana kipaji chake
 
Nilijua draft kipindi nina miaka 12 nadhani draft ni kipaji.
Kwanza draft haitakiwi ufikirie sana.
pili kabla hujasukuma kete mtazame usoni mpinzani wako.
Tatu kabla ya zamu yako kucheza usiangalie sana wenzako wanavyo cheza.
nne usicheze na watu wasio na viwango utadumaza kiwango chako.
 
Nimekulia uswahilini ,najua kucheza michezo mingi sana kuanzia Karata(Albastin/Mapiku) ,Draft(Nilikuwa najua kuingiza watu King) ,Bao la Kete ,Ukija Pool table au Zamani kulikuwa na Dude kama pool table lina wachezaji na michuma ,najua martial arts(Acrobatic) ,Kucheza Mpira(Football) etc kama ulikulia geti kali si rahisi kujua hiyo michezo.
 
Acha kumdanganya mwenzio.
 
Draft mara nyingi linachezwa na wanaume nyie kinamama hata msipolijua haina shida
 
mkuu hesabu za darasani na za draft tofauti kabisa ,Nikiendaga vile vijiwe vya draft nawakutaga jamaa vilaza tu kwenye hesabu alafu sisi tunaojua,log,matrix na ndugu zake kina probability tunafungwa tu binafs naupenda sana huu mchezo mpaka nimedowload game kwenye kitekno bt kila siku nafungwa tu.
 
Si kweli,wala hakuna uhusiano. Yupo jamaa nimesoma nae alikua dhaifu mno darasani, jamaa hata kuandika tu shida lakini ni mwamba wa drafti
 
Umeona?mpaka sometimes huwa nahisi draft ni kama kujua lugha au kuendesha baiskeli usipolijua utotoni inakuwa ngumu sana kulimasta ukubwani...ila ukishalijua hata usipocheza miaka 10 ukirudi inakuwa kama unakumbushia tu
Umenichekesha sana, mbona ni kitu rahisi sana hakihitaji hata kuanzishiwa mada
 
Kuna kipindi nikitulia huwa naona mpaka mchezo wa nne, nikiwa kawaida au sitaki kuumiza kichwa naishia mchezo wa pili tu
Kufikiria michezo minne mbele sio kazi rahisi, Mimi kuwa nafikiria 2 tu na pia siwezi kujiita Bingwa wa draft kabisa
 
Si kweli,wala hakuna uhusiano. Yupo jamaa nimesoma nae alikua dhaifu mno darasani, jamaa hata kuandika tu shida lakini ni mwamba wa drafti

Uhusiano upo tena mkubwa

Kuna watu wana akili sema wameaminishwa ni wajinga hivyo wameishi maisha yao yote wanaamini ni wazito darasani...

Namjua mtu ambaye alikuwa kati ya mwisho darasa la kwanza mpk la 5 halafu la sita na darasa 7 ndo anakuja kuwa kinara mnagombania nafasi za mwanzoni.Ni wasababu wamechelewa kujua uwezo wao


Kuna watu wana uwezo ila wanaamini hawana hao ndo wanakujaga kuwa wazuri kwenye draft wakati darasani ni wabovu.Kama unalijua draft vzr utakubaliana na mimi mwenye uwezo mdg wa kufikiria hawezi kuwa bingwa wa draft...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…