Twende hatua kwa hatua:
1. Tarehe za kujifungua inapimwa kitaalam kwa kutumia ultrasound kati za wiki ya nane na wiki ya 12 ya ujauzito. Iwapo hujapafanyiwa ultrasound katika muda huo, tarehe ya mwanzo ya siku zako za mwisho kabla ya ujauzito hutumika lakini hii ni iwapo uumekuwa ukiwa na siku regular. Kama siku zako ni irregular basi bila ultrasound tunaweza kusema kitaalam kuwa siku yako ya kujifungua haijulikani na tarehe zako zinaweza kutumika kwa sababu tu ndio the only available information although haina value kitaalam.
2. Iwapo mtoto aliye tumboni hana tatizo na iwapo afya yako iko vizuri. Operation haishauriwi kufanywa kabla ya kukamilika wiki 39. Kitaalam muda muafaka wa kujifungu ni wiki 38-40 za ujauzito, lakini muda huu ni kwa mtu anayejifungua mwenyewe bila operation wala kuchochea uchungu. Iwapo daktari anataka kukuinduce au kukufanyia opertion ilhali mtoto hana tatizo na wewe huna tatizo basi wiki ya 38 bado mapema, inapaswa asubiri angalau mpaka 39. Hivyo ndivyo inavyoshauriwa kitaalam.
3. Daktari wako wa kwanza ana uwezekano mkubwa zaidi wa kujua siku zako kuliko daktari wako wa pili kwa sababu yeye anaweza kuwa alikufanyia first trimester ultrasound inayoonyesha umri wa mtoto. Ultrasound za ujauzito ulikwishakua mkubwa hazionyeshi umri zinaonyesha ukuaji. Katika first trimester watoto wato wanakuwa sawasawa hata Hashima Thabit alikuwa na urefu sawa na
King Kong III katika umri huo, lakini ujauzito unapofika mwishoni tayari watoto warefu wanawapita wale wafupi hata kama umri wao ni sawa.
Lakini sasa, kama daktari wako anang´ang´ania tarehe hiyo na wewe mwenyewe umeshaamua kuhama basi itabidi umsikilize tu.
4. Kuna tabia ipo Tanzania mtu akiwa mjamzito anasafiri kwenda kukaa na mama yake eti ili aangaliwe vizuri. Tabia hii mimi siiungi mkono. Hakuna chochote unachotakiwa kuangaliwa ambacho unashindwa kukifanya nyumbani kwako. Kama hapa umeongeza uncertainity kwa kubadili daktari bila sababu ya msingi. Nikukuuliza ni nini unachoenda kufanyiwa na mama yako hutakuwa na jibu la moja kwa moja.
Zipo tabia nyingi zinafanywa ambazo haziadd value kwenye care ya mjamzito lakini zinaweza kuleta usumbufu na matatizo. Mfano mmojawapo ni tabia ya kuwakanda wazazi na maji ya moto!!! Mama wa wat wanaunguzwa bure for no good reason!!!
Kwahiyo
georgina george kuwa balizi mzuri kwa wajawazito wengine. Waambie wakae makwao wajfungue. Hawahitaji kusafiri wala kudafirisha mtu. Kama wewe umesafiri lakini unashinda JF, sasa JF ungekuwa kwako ungeishindwa?