Wakuu nimechanganyikiwa - daktari yupi yuko sahihi?

Duuuh, mbona roho inaanza kudunda! Wiki nzima sipati usingizi hasa kuanzia saa 8 usiku hadi saa 10 alfajiri.

Jichunge tu usipatwe na precipitated labour. Be calm mambo yote yatakuwa vizuri na utampata mwanao salama.
 
Hongera kwa umakini wako. Makadirio ya kujifungua kutumia tarehe za hedhi si sahihi sana. Ulishawahi kufanya ultra sound mwanzoni kabisa kabla ya miezi 4? Kama ndiyo,ilikuwa lini , ujauzito ulikuwa na wiki ngapi wakati huo? Halafu tuanzie hapo.
 
Huyo wa mwezi wa Tano aweza kuwa sawa. But ningeshauri ukafanye Ultrasound kwa uhakika zaidi.
Kipimo hiko chaweza kuwa na error ya wiki 2 zaidi au pungufu.
By the way, ulijuaje ujauzito wako ulifikisha ''wiki 34?'',
Tumia mahesabu hayohayo kujua tarehe ya operation/delivery!
 
Hiyo haina shida dada.mbona wengine mimba zinazaliwa miezi 11! Ila ikitokea emergence ukapata uchungu itabidi ufanyiwe OP siku hiyo hiyo.
 

Accuracy ya ultrasound baada ya wiki ya ishirini huwa inatofautiana kufuatana na kasi ya ukuaji wa mtoto tumboni.
 

kimanu, wewe ni daktari wa binadamu?
 
Last edited by a moderator:
Hongera kwa umakini wako. Makadirio ya kujifungua kutumia tarehe za hedhi si sahihi sana. Ulishawahi kufanya ultra sound mwanzoni kabisa kabla ya miezi 4? Kama ndiyo,ilikuwa lini , ujauzito ulikuwa na wiki ngapi wakati huo? Halafu tuanzie hapo.

Nope! Nilifanya U/Sound nikiwa na ujauzito wa week 28. Kama sikosei ilikuwa tarehe 3.3.2014.
 

Wote hawawezi kuwa sahihi kama wanataja tarehe tofauti
 
Twende hatua kwa hatua:

1. Tarehe za kujifungua inapimwa kitaalam kwa kutumia ultrasound kati za wiki ya nane na wiki ya 12 ya ujauzito. Iwapo hujapafanyiwa ultrasound katika muda huo, tarehe ya mwanzo ya siku zako za mwisho kabla ya ujauzito hutumika lakini hii ni iwapo uumekuwa ukiwa na siku regular. Kama siku zako ni irregular basi bila ultrasound tunaweza kusema kitaalam kuwa siku yako ya kujifungua haijulikani na tarehe zako zinaweza kutumika kwa sababu tu ndio the only available information although haina value kitaalam.

2. Iwapo mtoto aliye tumboni hana tatizo na iwapo afya yako iko vizuri. Operation haishauriwi kufanywa kabla ya kukamilika wiki 39. Kitaalam muda muafaka wa kujifungu ni wiki 38-40 za ujauzito, lakini muda huu ni kwa mtu anayejifungua mwenyewe bila operation wala kuchochea uchungu. Iwapo daktari anataka kukuinduce au kukufanyia opertion ilhali mtoto hana tatizo na wewe huna tatizo basi wiki ya 38 bado mapema, inapaswa asubiri angalau mpaka 39. Hivyo ndivyo inavyoshauriwa kitaalam.

3. Daktari wako wa kwanza ana uwezekano mkubwa zaidi wa kujua siku zako kuliko daktari wako wa pili kwa sababu yeye anaweza kuwa alikufanyia first trimester ultrasound inayoonyesha umri wa mtoto. Ultrasound za ujauzito ulikwishakua mkubwa hazionyeshi umri zinaonyesha ukuaji. Katika first trimester watoto wato wanakuwa sawasawa hata Hashima Thabit alikuwa na urefu sawa na King Kong III katika umri huo, lakini ujauzito unapofika mwishoni tayari watoto warefu wanawapita wale wafupi hata kama umri wao ni sawa.
Lakini sasa, kama daktari wako anang´ang´ania tarehe hiyo na wewe mwenyewe umeshaamua kuhama basi itabidi umsikilize tu.


4. Kuna tabia ipo Tanzania mtu akiwa mjamzito anasafiri kwenda kukaa na mama yake eti ili aangaliwe vizuri. Tabia hii mimi siiungi mkono. Hakuna chochote unachotakiwa kuangaliwa ambacho unashindwa kukifanya nyumbani kwako. Kama hapa umeongeza uncertainity kwa kubadili daktari bila sababu ya msingi. Nikukuuliza ni nini unachoenda kufanyiwa na mama yako hutakuwa na jibu la moja kwa moja.
Zipo tabia nyingi zinafanywa ambazo haziadd value kwenye care ya mjamzito lakini zinaweza kuleta usumbufu na matatizo. Mfano mmojawapo ni tabia ya kuwakanda wazazi na maji ya moto!!! Mama wa wat wanaunguzwa bure for no good reason!!!

Kwahiyo georgina george kuwa balizi mzuri kwa wajawazito wengine. Waambie wakae makwao wajfungue. Hawahitaji kusafiri wala kudafirisha mtu. Kama wewe umesafiri lakini unashinda JF, sasa JF ungekuwa kwako ungeishindwa?
 
Last edited by a moderator:

Mkuu, zipo sababu nne za msingi zilizofanya nisafiri japo siwezi kumwaga kila kitu hapa jamvini. Ninashukuru kwa ushauri.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…