Mtangazji wa runinga na redio nchini Tanzania, Farhia Middle, amesema tangu aingie katika ulimwengu wa mapenzi hajawahi kukutana na mwanaume mwaminifu na kudai kuwa mara kwa mara amekuwa akilizwa na mapenzi jambo ambalo anajiona kama mtu mwenye mkosi.
Akihojiwa amesema kuwa licha ya kusifiwa kwa uzuri na muonekano wake bado amekuwa akikutana na balaa kwa wanaume wasio waaminifu na wanaume wenye mfumo dume wa kuwanyanyasa wapenzi wao jambo ambalo linaendelea kumuumiza katika mapenzi.
Amesema kuwa kuna muda huwa najiuliza ana mkosi gani mbona kila siku analizwa yeye tu? na kudai kuwa anajiona ana mkosi kwani kila mwanaume atakayempata hadumu naye, kitu ambacho kinamuumiza sana na kumkoseshsa raha katika maisha ya mapenzi.