Baadhi ya watu wanapata tatizo kuelewa maana ya 'hisa'. Mada hii inachanganua. Tuanze na mfano rahisi wa biashara. Tuchukue mfano wa mradi daladala, tuuite,
JF Trans, kwa madhumuni ya hoja hii.
Tuchukulie tunataka kununua
minibus inayogharimu shilingi milioni hamsini, Sh 50,000,000/= Tuchukulie "hesabu" ya "tajiri" ni shilingi laki moja (100,000/=) kila siku.
Picha ya kwanza:
Mtu mmoja akifanya maamuzi magumu na kununua gari hiyo, atatoa shilingi milioni hamsini zote yeye peke yake. Na "mpunga" wa hesabu atauchukua peke yake kila siku.
Picha ya pili:
Wakiwa watu wawili waliowekeza milioni ishirini na tano kila mmoja kwenye kununua basi, kila mmoja atakuwa na umiliki nusu wa basi hili.
Swali 1.: mpunga wa "hesabu" kila siku kila mmoja atachukua kiasi gani? ___________.(
Hinti: nusu bin nusu).
Picha ya hisa:
Tuchukulie kwamba yupo mtu mzoefu kuendesha madaladala. Lakini kutokana na 'ukapa' akawa hana nguvu za kununua gari hilo peke yake. Labda ameweza kukusanya mtaji wa shilingi milioni kumi tu. Kwa hiyo, lengo la kupata milioni hamsini limetimia kwa asilimia 20 tu. Ili kupata milioni arobaini zilizobaki anaamua kuuza asilimia 80 ya umiliki wa gari hilo, yaani shilingi milioni arobaini.
Kwa kujua hali ngumu iliyopo, akaamua 'kuvunja' hiyo milioni hamsini ya basi iwe vipande elfu kumi
vilivyo sawa. 50,000,000 / 10,000 = 5,000.
Swali 2: Kwa vile yeye tayari ashaweka milioni kumi kwenye
JF Trans, je anamiliki vipande vingapi?________ (
Hinti: milioni kumi gawa kwa sh elfu tano).
Vipande vilivyobaki bila mmiliki ni 8,000. Kila kipande (hisa) sh 5,000. Thamani Jumla Milioni arobaini.
Hapo sasa inatolewa ofa kwa jamii. Tuseme hisa moja inatolewa ofa ya awali kwa umma (
Initial Public Offer, IPO) ya kuuzwa sh 7,000. Jumla ya hisa ni 8,000. Kiasi cha chini kununua ni hisa kumi. Yaani Sh 70,000. Ukinunua zaidi, unaweza kuongezea hisa tano tano (elfu 35).
Swali 3. Mategemeo ya makusanyo yatakuwa shingi ngapi? _________ (
Hinti: idadi ya hisa zinazouzwa x bei ya hisa.) Tuchukulie hisa zote elfu kumi zimepata wanunuzi.
Jamaa anakuwa mkononi na mtaji wa shilingi
milioni 66. Ikiwa tuko wote mpaka hapa, mambo safi. Vinginevyo, fanya
homework 😉 hiyo hapo juu vizuri.
Jamaa anachukua milioni hamsini ananunua basi. Milioni kumi na sita anatia mfukoni kama faida / gharama za kuanzia biashara.
Swali 4: Biashara ikianza, kila siku mwenye hisa anachukua shilingi ngapi kwa kila hisa? _________________
Swali 5: Itachukua siku ngapi gawio la hesabu kurudisha gharama ya hisa? ______
Swali 6: Aliyeanzisha mradi (20% hisa) atakuwa anachukua shilingi ngapi kila siku?_______
Swali 7: Hisa hizi zingeuzwa kweli, ungenunua ngapi?
😀 ____________
Mfano huu umerahisishwa kupunguza '
variables'. Halafu miye si mtaalamu niliyesajiliwa wa hisa
🙁
Update 1: Soko la Hisa
Baada ya muda, ile ofa ya awali yenye bei moja itafikia mwisho. Baada ya hapo, hisa zitakubaliwa kuuzwa kwenye soko la hisa, ili kuwapa fursa wasiokuwa nazo kuzipata, na walionazo kuziuza.
Kwa mfano wetu, tuchukulie mtu aliyenunua hisa 100 za awali kwa bei ya shilingi 5,000 hisa moja. Akiamua kuziuza hawezi kuzipeleka sokoni kwingine, bali kwenye soko la hisa. Hapo mawakala wataanza kuzinadi, tuseme, kwa bei hiyohiyo ya sh 5,000. Wateja
AMA watazigombea
AU watazikacha. Wakizigombea, bei itapanda, kwa vile zinauzwa kwa mnada. Wakizikacha, bei itashuka.
Ukiwa unamiliki hisa za JF Trans, na taarifa ya habari saa mbilli usiku imefikia mahali inasema,
sasa tunawaletea mauzo yalivyokuwa kwenye soko la hisa leo hii, hutabadili chaneli kwa vile
kwako wewe taarifa ishaisha, bali utasikiliza vizuri ili ujue
uwekezaji wako unaendaje. Bei ikipanda, mfano toka sh 5,000 kwa hisa, na kuwa sh 6,000, ukiuza hisa zako 100 utakuwa umepata faida ya sh (100 x 1000) 100,000.
Ila bei ikishuka, na kuwa sh 4,000 hisa ulizo nazo zitakuwa zimeshuka thamani, na ungeziuza kwa siku hiyo ungepata hasara ya sh 100,000 kutoka kwa bei uliyonunulia.
===
Pamoja.