Hisa za Vodacom zipo vipi?
Wengi miongoni mwetu tumekuwa tukitaka kujua kuhusu HISA za Vodacom na hii imenifanya nitupie jicho niwape ubuyu kidogo juu ya hisa hizi kwa faida ya wengi.
Kwa tafsiri rahisi HISA NI UMILIKI.
Hii inaamanisha kampuni ya Voda imetoa nafasi ya umiliki kwa wateja watakaonunua hisa za awali.
Mtu akisema nina hisa Vodacom anamaanisha anamiliki Vodacom. Umiliki huu unajionyesha wazi na bayana wakati wa kufanya maamuzi na kugawana gawio (faida inayopatikana katika kampuni). Mwenye hisa nyingi huwa na sauti au ushawishi mkubwa katika kufanya maamuzi na hupewa gawio kubwa kwa uwiano wa hisa zake lakini hakuna upendelo unatokana na upendeleo ya Idadi ya hisa unazomiliki.
Mfano Kama unamiliki hisa 100 za Vodacom Tanzania zitakufanya uwe na haki ya kuwa na kura 100 ktk Mkutano Mkuu wa Mwaka.
Kampuni ya Vodacom asilimia 65 ya hisa zinamilikiwa na Vodacom Group na asilimia 17.5 zinamilikiwa na Mirambo Limited kwa hiyo hii 25% ya hisa zilizowekwa kwenye ofa ni makubaliano Kati ya kampuni ya Vodacom na Mirambo kutoa idadi ya hisa 560Milioni sawa na hizo asilimia 25 Mwenye kuweza kununua hisa milioni 230 atakuwa amenunua hisa nyingi zaidi kuliko yeyote na anakuwa na nguvu ya maamuzi katika vikao na gawio atapata kubwa kwa sababu ndie aliechangia mtaji mkubwa.
Faida za kuwa na Hisa za Vodacom:
1. Unapata fursa ya kuwa mmoja ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ama moja kwa moja au kwa kuwakilishwa.
2. Mwanahisa anapofariki shughuli za kampuni haziwezi kuyumba kwa sababu jukumu la kazi za kila siku lipo mikononi mwa menejimenti najua kuna watu wanahofia Hisa zangu ndiyo zimefika mwisho hapana suala la uendeshaji lipo mikononi mwa Menejimenti.
3. Ni rahisi zaidi kuuza HISA pindi unapoona hauhitaji kuendelea na umiliki na ukitaka kuziuza tafuta kipindi ambacho bei ipo juu ili ufaidike bei ya Ofa inaweza kuwa ndogo kulinganisha na ile ya kuingia kwenye soko pale bei inakuwa juu muda wa ofa Kama huu ndiyo mzuri kununua Hisa.
4. HISA ni dhamana (badala ya kuweka nyumba/shamba ili uweze kukopeshwa na taasisi za fedha waweza kuweka dhamana ya hisa zako).
5. Kampuni inapofanya vizuri sokoni ama kwa kutoa huduma/bidhaa bora au kwa kuwa na mipango mkakati mizuri thamani ya HISA hupanda. Unaweza kununua Leo kwa 850 then bei ikapanda hadi 2000.
Kwa maana hiyo mbali ya gawio mtu anaweza kuuza hisa kwa bei inayomlipa akilinganisha na bei ya kununulia.
Ni wakati wa kuchangamkia Fursa hii asee ofa imebaki muda mfupi kufungwa.