Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kuna mzee mmoja alinishauri. na kuniambia; kijana, sikiliza ushuri wangu, kwa sababu nimekula chuvi nyingi; katika maisha yako ya mapenzi:-
- Hakikisha unakuwa na mahusiano na mama ntilie;- ili siku utakapokuwa na njaa, na huna sehemu ya kupata chakula, atakuhudumia.
- Hakikisha unakuwa na mahusiano na nesi:- ili siku utakapopata matatizo ya kiafya aweze kukusaidia.
- Hakikisha unakuwa kwenye mahusiano na askari:- ili pale utakapokamatika uweze kupata mtetezi.
- Hakikisha unakuwa kwenye mahusiano na daktari:- ili pale utakapohitaji matibabu akusaidie.
- Hakikisha unakuwa kwenye mahusiano na hakimu:- ili pale mambo ya kisheria yatakapohitajika akusaidie.
- Hakikisha unakuwa kwenye mahusiano na mwalimu:- ili aje akusaidie kuwalea watoto wako kwa kuwapa elimu bora.