Wakuu ushauri wenu katika changamoto ya kuendesha gari

Mimi sina shida na hii part ya manual,shida yangu ni kuwa je ninaweza kupanda milima yote kwa kutumia D peke yake bila ya kucheza na hizo + and - ?(manual)

Jibu ni ndio( Kwani umeona magari yote yana auto manual kama yako) ??? mengine hayana na yanapanda milima. D tumekuambia inacheza na gia zote kutokana na hali ya Acceleration. ila wakati wa kushuka ndio nimekushauri tumia manual ili gari isikimbie. pia Itakula sana mafuta maana RPM itakua juu mmno
 
Sasa kaka nikitaka ligi na mtu si ninaweka overdrive(OD)?Tofauti ya S na OD ni nini?

Daaaaaaaaah kaka gari sio lazima iwe na option zote. mfano mm gari yangu haina O/D na hizo S

OD ni overdrive hii inafanya Gari kuwa na nguvu/ na spiid na ulaji mzuri wa wese.

Na S ni sport nayo inaongeza uwezo wa gari lakini inatandika sana ngwese maana Gari yenye S pia inasehemu ya Economical ili kupunguza consuptuin ya wese
 
Watu wengi wasichokijua ikiwa ni pamoja na wewe ni kwamba S siyo gear ya kukimbia.S ni gear ya kupandia barabara refu na yenye milima midogo yenye kona nyingi lakini katika barabara nzuri au barabara ya kawaida lakini yenye umbali mrefu na yenye konakona nyingi,yaani S ni kama gear namba 3 ndiyo maana huwa inakula mafuta.Watu wengi huwa wanafikiri S ni gear ya kukimbia a.k.a gear ya ligi kitu ambacho siyo sahihi!Gear ya kukimbia haipaswi kula mafuta mengi.
 
Maisha yako yote unatakiwa ujue ligi ni mafuta mengi, unless gari iwe electric!

Usidanganywe eti gear kwa ajili ya mbio inatakiwa isitumie kiasi kikubwa cha mafuta..



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…