Wakuu ushauri wenu ni muhimu, nimefilisika

[emoji122]
 

Mkuu na wewe chanzo ni kumiliki gari tu ndio mwanzo wa kuanguka?
 
Awali ya yote, naomba nikupe pole mkuu kwa hayo unayoyapitia!

Ila ninafurahi kuona still you're strong, hakika ni watu wachache sana, wanaoweza kuendelea kuwa +ve kwenye viatu vyako!

Ushauri wangu:
Hapo ulipo, naona best alternatives zote unazo! But unatakiwa UTULIZE TU AKILI....for sure utatoka hapo ulipo, kama matani vile!

All the best chief.
 
Ndugu yangu pole sana brother,
Kaka wewe bado ni tajiri kwa nn unakata tamaa?
Angalia ulipojikwaa usiangalieulikoangukia
Wapo wengi huangushwa na Mungu kisha huinuliwa upya na kuvikwa uimara dhabiti
Kaka angalia sababu za kufikia hapo kisha jipange upya

Ibada+bidii=mafanikio

Nakutakia kila la kheri
 

Kumiliki BMW mpaka bodaboda ni kweli? Au ndo ngano za kiswahili.

imebidi nijaribu kuitafuta angalau inayofanana.
mkuu inawezekana kabisa unaamua kuuza ili uongeze mtaji katika biashara na ghafla inakata unafanyaje? naelewa watu wengi waliokuwa na mawe na wakaanguka
 
hongera sana kwa kujianika hapa!
uzi umetufaa wengi tulioandika na wasioandika na wapo wengine watasimama tena kwa ajiri ya uzi huu hongera sana kwa kupata kibali na kujifunua na pia wadau walioweza kutoa ushauri mbalimbali katika uzi huu.
nafikiri uliona kuwa huna shati lakini wadau wamekuonyesha shati umevaa ila hujachomekea tu!
sasa na mimi nianze kukushauri kwa kadri ninachofikiri naweza.
  1. kwanza usikate tamaa yupo mzee alipata utajiri akiwa na umri wa miaka 75 na mpka sasa bado yupo na akaoa mke mwingine anakula hela yake umri huo alikuwa nao mwaka 2004 sasa unaweza kuona ana umri gani 30 kitu gani kwako?
  2. wengi tutakuelekeza jinsi ya kusimama lakini leo tubadili tukuelekeze kwanza wapi ulianguka ili usianguke tena
    1. matumizi yako yalikuwaje? kama yaliongezeka kuliko kipato lazima uanguke kipindi cha selikali hii purchasing power kwa watu wengi imepungua kiasi kuwa watu wengi wamekuwa wanunuzi wa vitu muhimu na ziada wananunua kwa kiasi kidogo pale inapobidi sasa kama unafanya biashara ya vitu visivyo vya lazima lazima mauzo yashuke lakini wakati huo huo mke anakwambia hataki kusikia umewatoa watoto English medium school kwa hiyo lazima ule mtaji.
    2. shughuli za udalali zinaendana na dili kiasi kwamba kwa kipindi hiki zimebaki chache na udalali huwa wanamatumizi makubwa sijui kwanini sasa zikikata lazima ziyumbe. lakini pia kwa kazi hiyo hiyo inawezekana mliwadhurumu watu wakaweka kinyongo kwa njia moja au nyingine nafsi zinazolalamika huaribu mafanikio kwa njia moja au nyingine.
    3. uchaguzi mbovu wa biashara ni chanzo pia cha kutofanikiwa. yako mambo mengi lakini yakuzingatia lakini vifuatavyo vinaweza kuwa msaada kwako
      1. ujuzi na maarifa pia muda wa kufanya shughuli uliyoichagua kuna uwezekano haukuwa na maarifa ya kutosha na muda wa kutosha kuifanya biashara uliyoichagua hivyo kukufanya kuiendesha kwa gharama kubwa sana kuliko mapato
      2. soko la bidhaa ulizokuwa unauza lilikuwaje na hapa unaangali uhitaji wa bidhaa na wauzaji wengine ukoje na wauzaji wengine wanakuzidi nini na wewe unawazidi nini na unabadilikaje kurikabili soko
      3. upatikanaji wa faida ukoje? si swala la kununua bidhaa 900/- na kuuza 1200/- je gharama gani zinaendana na uendeshaji wa biashara wengi hawahesabu gharama za mafuta ya gari chakula mchana na vocha za simu kama zinahusu biashara.
      4. mtaji uliwekaje? kuwa na mtaji mkubwa au mdogo husababisha pia kuanguka kwa biashara mfano wafanyakazi wengi wakianzisha biashara wanaweza wasione faida au hasara kwa kuwa huwa wanajikuta wanashindwa kutenganisha fedha binafsi na za biashara. pia wengine wanashindwa kutenga au kujua mtaji unaohitajika katika uendeshaji na vifaa vya kudumu over investment ni shiiida kwa biashara.
      5. kiasi gani ulipanga biashara igharamie mahitaji ya familia yako
    4. baada ya kuona vigezo vya kuchagua la msingi sasa lazima tuangalie jinsi ya mpangilio sikawa shughuli zote lazima kujua zipi ni za mwanzo kabla ya kuanza biashara na pia kuanzia ununuaji/uzalishaji mpaka uuzaji kipi kinaanza na kitahitaji kiasi gani cha fedha
    5. usimamizi ni muhimu ulismamiaje biashara yako na wengi tunakwama hapa
      1. usimamizi wa fedha za mauzo - mfano ukiwa na duka au daladala familia ikihitaji fedha ya dharura kwa haraka tegemea wewe kuhusika sasa je ukishatoa unarudisha?
      2. usimamizi wa mikopo
        1. mikopo ya bidhaa
          1. mikopo kwa wateja; hatuwezi kuuza bila kukopesha lakini tuelewe kwamba tunapokopesha tunawagharamia wateja na tusipokuwa makini tunapunguza mtaji wa kujiendesha bila kujua sasa je tumeweka kiwango cha mwisho cha kukopesha wateja? hivyo mikopo huangusha biashara.
          2. mikopo kwa waleta bidhaa hii inahitajika lakini wakati mwingine inaweza kusababisha ufuatiliaje mbovu kwa madeni ya wateja pia utumiaji mbovu wa bidhaa ghafi. pia malipo kwa wanaoleta bidhaa ni muhimu wakalipwa kwa makubaliano ili waendelee kuleta bidhaa.
        2. mikopo ya fedha kwenye taasisi za fedha na mikopo gharama zilikuwaje za mikopo kuna uwezekano riba zikasababisha kuanguka kwa biashara madeni yakizidi husababisha biashara kuanguka
      3. jinsi gani ulijipanga kwa dharura zisizo tarajiwa risk management hii ni shiiiida mfano kwa wale wanaofanya biashara ya kukopesha vijijini wameathirika kwa kiasi fulani na fedha za Magufuli huko kijijini
yapo mengi lakini kwa kuanzia hiki kinaweza kukusaidia baadaye nitakuja na success story nini kipo katika game.
 
Hapo kwenye madeni pananihusu sana, Niko kwenye sama situation nanahisi safe plan kwasasa nikutoyalipa ila napata stress sna kufikiria jamaa watanielewaje
Mimi mbinu niliyotumia ni hii.
Taasisi zinazonidai hizo nakomaa nalipa zote bila kukopa tena yaani kama ni CRDB au Brac nikulipa na kufuta deni kabisa.
Haya madeni ya washkaji, yaani ya boss niazime 500,000 kesho narudisha, hizo kiukweli nimejumlisha maden ya wana yote nimejua nadaiwa sh kadhaa, nimewaweka jamaa pending tena kwa kuwaambia ukweli (samahani kaka sitaweza kukulipa sasa hadi wakati nikikaa poa hata kwa riba).
Aelewe asielewe nitakuja walipa kwasasa nakomaa kusimama
 
Mkuu pole sana.. Nilikuwa nahisi mimi pekee ndo muhanga wa kutoka class ya juu kwenda chini ila kupitia story yako nimejiona nipo kwenye right track.
Bro yaani mimi kwasasa nimejipa moyo tu. Nilikata tamaa sana hadi sumu nimekunywa, lakini kwasasa tuambiane tu ukweli si pekee etu tupo wengi hivyo tujikaze.
Then watu wanafikiri kufilisika ni jambo gumu sana.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Hawajui inaweza ikawa ni dakika tu.
 
Mkuu kubali hali iliyopo, sahau ulichokuwa nacho anza upya. Kama Kuna fursa ya kufanya na inahitaji mtaji usisite kuuza hicho kiwanja kwani Kila kitu tulicho nacho tuko nacho kwa sababu tulikitafuta palipokuwepo na fursa, suala la mambo kwenda kombo wala siyo mkosi, maana wakati tunakuwa nacho Kuna wengine wanakuwa hawana hivyo ni hali ya mzunguko wa Maisha. Tujifunze kushughuri kwa Kila Khali.
 
Daah maisha weeee, haya in mapito tu na tumepitia wengi, utavuka
 
Hii awamu waliokuwa wanaishi kwa dili (kama madalali) wanaisoma namba sana. Kwa ufupi hauko peke yako anguko hili ni kwa wengi kama walivyoeleza waliotangulia ni kwamba kwa jinsi hali ya Maisha ilivyo ngumu watu wamepunguza sana matumizi yasiyo ya lazima na pesa imekuwa ngumu sana. Siku hizi mahoteli hayana wateja wazinzi na wasafiri wamebadilisha sehemu za kulala wanalala kwa ndugu zao na wazinzi wamewarudia wake zao. Vituo vya mafuta haviuzi, Maduka ya nguo hayauzi, vyakula vya anasa watu hawala, baa zimepunguza mauzo, taxi hamna abiria, yaani kila kona watu wanalia maumivu hauko peke yako mzee baba. Kila mtu kachoka kwa namna yake
 
Tatizo la waafrica wanakata tamaa haraka sana miaka 30 tuu umejikatia tamaa,,anzia ulipo songa mbele mtegemee mungu achana na waganga njaa hao ndo chanzo cha wewe kurudi nyuma.never giver up man.
 
Yaan kunawakat naona nikama maisha yananilazimisha nitembee juu ya maji bila kuzama
 
Mtaalam wa Saikolojia mwenyewe anategemea hela za wenye msongo wa mawazo ndo aishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…