Wakuu ushauri wenu ni muhimu, nimefilisika

pole sana kaka usikate tamaa.
 
Mkuu Mshukuru Mungu sana kwa maana bado kakupa akili ya kushtua ubongo wako mapema hivyo nafasi bado unayo, Tatizo unaingiza hofu ya kushindwa mapema.

Pia nirudi nyuma angalia kwenye maisha yako ya nyuma au ya udalali kuna mtu huenda ulimdhulumu kwa namna moja au nyingine?

Madalali mnakuwaga na katabia fulani siyo kazuri..... Piga maombi mlilie Mungu yatakwisha, tukisema kila mtu aandike hapa uenda wewe uko afadhali!!. [emoji3447]
 
Ushauri.. usiende kwa mganga tena
 
Mtoa mada cheki huu uzi hapa chini unaweza angalau kukutia moyo na ukajua unayoyapitia hauko peke yako mkuu.

Ni uzi poa sana.

 
Uvuvi ulikuwa unafanyia sehemu gani?
Kama bado una engine za mitumbwi uwezi kulala njaa kwa Dar unaweza ukawa unaikodisha kwa siku sh 15000.

Pia kama una mitumbwi mingi ya mbao iuze baki na mashine kisha nenda Pangani ukawekeze kwa kununua fiber boat hata ya million 7. Engine utafunga ulizonazo.

Pangani utafanya biashara ya kubeba watalii boti zipo chache sana. Ukiwa na fiber utakodishwa kwenda Zanzibar na kwa mtalii 1 bei ni dolla 25.

Ukiwa pale pale Pangani utabeba watalii wa ndani na nje kuwapeleka Mauya kucheki mamba na wengine kuwazungusha baharini.
 
Kumiliki BMW mpaka bodaboda ni kweli? Au ndo ngano za kiswahili.
Ah..unashangaa ki BMW? nina jamaa yangu ilikuwa anaishi kigamboni mjengo wa maana ana malori ya mchanga saa hz dereva Dangote ninachomkubali tu yule mwamba huwa havurugwi anajua sana kujiposition na kwa spidi yake ipo siku atarudi kwenye mstari maana anapiga udereva huku anafanya biashara japo mtaji si mkubwa ila ile spirit yake inambeba halikatagi tamaa lile jamaa sijui limeumbwaje!
 
Wengi tumepitia huko ila hakuna kukata tamaa, sahivi mambo mukide mukide, amini nakuambia sasa hivi utanyanyuka
 
USIKATE TAMAA. Mweke Mungu mbele. Kaa na mkeo mweleze yote mpeane mawazo. Lakini mfanye sala na dua sana Mungu atafungua tu njia. Hao marafiki zako uliowapata kwenye utalii waambie unataka kuanza biashara ya kuwauzia vitu vidogo vidogo ambavyo watalii wanapenda- batiki, vinyago, n.k. Wakutumie hela uwapelekee. Unaweza kushangaa ukianza na ka mtaji ka laki moja "UTATOKA" Kikubwa USIKATE TAMAA na mwamini Mungu
 
Ni kama vile uko ndotoni kuna mda nawaza ivi Mimi ndie yule kevi niliekuwa nauwezo wa kutumia laki kwa siku. leo Hii nikitumia elfu 5 najitafakari.
 
Kweli maisha ni fumbo la imani yakigeuka mpaka mwenyeWe unajishangaa Mimi mapito yangu nimeandika kwa ufupi sana kuna mengi sana ndani yake nimepitia starehe nikiwa na miaka 16-19 nakaa na watalii kutembelea maeneo ya utamaduni mbuga za wanyama na Bata tu asubuhi mpaka asubuhi. iyo ikapitaga baada ya kufeli kupata visa ya USA nikaona bora nikasome zangu chuo nikaacha utalii.

nkafunguaga asasi nikaachana nayo baada ya kufanya registration nikafanya airbnb nikatulia nikapiga day worker kama sales nyota ikangaa nikanunua vitu vitu budget ya home kwa siku ikawa ni 35k extended family. Mambo yakawa hot....nikapiga mazao....Ukiwa na pesa unaweza kufanya vitu..vingi.sana au niseme unaweza kufanya chochote kila muda naamini.utajiri ni SIRI iko siku pesa zitanirudia tena kwa kasi sitoziruhusu ziiondoke tena
 
Maisha haya acheni,kama mm ups and down za kutosha,madeni ndio usiseme ila kukopa kwangu ni katika harakati za kutaka kujiinua tena na nina amini nikiinuka sitarudi chini Inshaallah,ila ndg ukiwaamini na kiwakabidhi biashara kukuangusha ni faster
 
Kama ukiangalia vizuri..kosa lilianzia kwenye kuoa...!!

Kama walau ungesubiri kidogo naamini ungkuwa mbali

Vijana tukianza kufanikiwa mengi huja kichwan....!!lakini hasa huja la kukaa na mwanamke ndan...!!sio ubaguzi....lkn inashauriwa pale kabla ya kuoa hakikisha umepata chanzo cha kudumu cha pesa na pia makazi ya kudumu

Lakn pia tusiharakishe mambo kwa haraka bali kaa na mtu ukimsoma na mkipanga maisha.

Tengenezeni maisha yenu pamoja....andaeni future ynu na watoto kisha mambo mengne yafuate

Ila pia angalia na aina ya mwanamke....!!ukikosea tu mke....ndugu utauza ufuta mpk popo wtakucheka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…