Wakuu wa Mikoa wapewa kazi ya kuwashughulikia wanaopandisha bei ya vyakula kwenye mfungo wa ramadhani

Wakuu wa Mikoa wapewa kazi ya kuwashughulikia wanaopandisha bei ya vyakula kwenye mfungo wa ramadhani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
6da7389bbf3bf2271cfa2e8b6f2fceb5
Wakuu wa Mikoa kote nchini wameagizwa kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuuza sukari kwa shilingi 4500.

Waziri Mkuu Mhe.Kasim Majaliwa amesema hakuna sababu ya sukari kupanda bei kwani sukari ipo yakutosha, ilikuwa imepungua imeagizwa na imekwishaletwa.

Majaliwa ameyasema hayo leo Jumatano April 22, 2020 akiwa kwenye Maombezi ya kuombea Taifa dhidi ya ugonjwa huu yanayofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar

“Wiki hii waumini wa kiislamu wanaanza mfungo wa Ramadhan hivyo natoa wito kwa wafanyabiashara kuhakikisha vyakula muhimu vinauzwa kwa bei ya kawaida, Wakuu wa Mikoa na Wilaya wafanye ukaguzi mara kwa mara kwenye masoko ili kuhakikisha bei ni ile ile.

"Hakuna sababu ya bei ya Sukari kupanda, Sukari ipo tena ya kutosha, ilikuwa imepungua imeagizwa na imekwishaletwa, nawaagiza Wakuu wa Mikoa yeyote atakayeuza Sukari kwa Shilingi 4500, chukueni hatua kali dhidi yake" Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
 
Mmeletewa shehena ya vifaa kupambana na corona mmefungia hadi ghala limewaka moto, msijifiche kwenye vitu vidogo vidogo.... sukari sio lazima.
 
.....soko la Kariakoo litafanya kazi kwa Masaa 24 kuanzia Mwezi mtukufu wa Ramadhan....
 
Mbona kama naona mauzauza. Sasa bei halisi ya Sukari ni Tshs ngapi kwa Kilo.

Waziri Mkuu angetoa bei Elekezi ya Kuanzia na Mwisho.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom