Wakuu wa Ofisi za umma zinazonyima wananchi huduma kisa Corona au kutovaa barakoa, wafukuzwe kazi

Wakuu wa Ofisi za umma zinazonyima wananchi huduma kisa Corona au kutovaa barakoa, wafukuzwe kazi

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Mkuu ameshatoa agizo watu wachape kazi, yeye mwenyewe havai barakoa.

Sasa kuna ofisi za umma zinanyima huduma wananchi kisa hawajavaa barakoa, hawa wafutwe kazi.

Jaji Mkuu na majaji wenzake na mahakimu wametengeneza genge la ulaji, wananunua TV kama wamechanganyikiwa, huu ni ufisadi mkubwa, eti wanazitumia kusikiliza kesi, ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi wakati mahakama nyingi hazina vyumba.

Kuna mahakama ambazo wanapiga tarehe juu kwa juu, tena kupitia karani.

Ofisi za umma ziache ubabaishaji, hapa kazi tu.
 
Jana nilipita mahakama moja wafanyakazi wanategea sana kazini. Majaji hawapo wala hakimu.
 
Vaa barakoa; acha upunyenge wako! Wafukuzwe kazi wataalam kisa kiazi lisilovaa barakoa? Unashindwa kufunga hata kitambaa au tishu? Au unazan ofisi za umma zinahudumiwa na roboti?
 
Jana nilipita mahakama moja wafanyakazi wanategea sana kazini.
Majaji hawapo wala hakimu.
Idara ya mahakama bado hovyo tu, hapo ukiwapa elfu tano watachangamka kukuhudumia
 
KUNA WATU WAMEAMBUKIZWA ROHO MBAYA HUMU NDANI
 
Vaa barakoa; acha upunyenge wako! Wafukuzwe kazi wataalam kisa kiazi lisilovaa barakoa? Unashindwa kufunga hata kitambaa au tishu? Au unazan ofisi za umma zinahudumiwa na roboti?
Nakushuru baba mchungaji kwa kutovaa barakoa-Mkuu.
 
Back
Top Bottom