Wakuu wa Vyombo: Mnasubiri ya Zimbabwe na sisi Tanzania yatufike?

D

DeletedMember281674

Guest
Kilio changu na kupeleka kwa wakuu wa vyombo tunashindwa Nini? Mbona Zimbabwe waliweza kumuweka pembeni Mzee Mugabe.

Tanzania ni kubwa sana kuliko kumlinda mtu Mmoja tukafikishana kununua mkate kwa Shilingi laki Moja tuanze kujikuta tunatumia Shilingi ya Kenya kwenye uchumi wetu ni vyema tu akapisha au kaka pembeni kabla Hasira za wananchi kutokea hiyo December 9.

Amezika Ndugu zetu kibabe Sana. Na D9 wataandamana kudai Ndugu zao wafukuliwe wakawazike kwa heshima. Je mtawapa hiyo Miili? Au mtawaua kuongeza maumivu na Hasira


Leo hii kila Kona Bunge la Ulaya limepitishq vikwazo dhidi ya Tanzania bado USA, hii Ina maana watali na wawekezaji tusahau.

Sasa hivi watu mkiwafungia habari ndani ya nchi yao wanapata kupitia mitandao ya jamii na Television za nchi jirani.

Sasa kwanini tuendelee na huu ujinga??? Au mnataka tuamini Kwamba kawahonga na ndiyo mpo toothless na mpo tayari kututeka na kutuua???
 
Mtoa mada kama unaweza kuukata mkono wako unaokusaidia kula msosi, basi ndivyo hivyo hivyo kwa hao wakuu wa vyombo vya dola.

Kifupi hao wote ni chawa tu wasioweza kwenda kinyume na bosi wao aliyewateua. Hata nchi itumbukie shimoni, na wenyewe watatumbukia, au kukimbilia nchi nyingine. Ila siyo kufanya hayo maamuzi unayo yawazia.
 
Wafanye haraka kabla mambo hayajaharibika zaidi. Inasikitisha.
 

Tuendelee kusoma visomo vyetu ili parapanda ilie na bendera nusu mlingoti iweze kupandishwa mapema kabla Mwaka huu haujaisha

Kapora uchaguzi na uhai wa Ndugu zetu na mbaya zaidi kawafukia kibabe na bado anajizima data Kwamba wananchi walimchagua huku walikuwa hawamtaki ameshindwa KUSIMAMIA RASIMALI za nchi ili ziwanufaishe watanganyika katika kuwapa fursa za Ajira na kupunguza ugumu wa Maisha kwa wananchi yeye anakula tu kwa urefu wa Kamba yake na Abdul na kuendekeza tamaa na ufisadi uliokithiri na kutulingishia walipa Kodi wake na Rolls Royce na dharau zake za nywi nywi nywi nywi

Bado anatuteka na kutuua wananchi ili kutujengea hofu wananchi tukae kimya na tuzidi kumuogopa

Huyu Shetani mla damu hajielewi Dunia ilipofikia Sasa hivi hakuna mtu atakayeogopa kutekwa na kuuwawa au hizo risasi. Kama anafikiri hayo mambo anayotafanya ya Kuteka, kuua na kupiga watu risasi na kawafukia kibabe vitamsaidia basi anajidanya.

Acha tuendelee na visomo vyetu kwa MUNGU wetu Mwaka huu usiiche akalale anapostahili akutane na huyo Shetani wake aliyemtuma kutoa oda ya shoot to kill.
 
vyombo gani..kwani 29/10 hadi 03/11 havikuwepo..? hivi tukio la kuua watu hawakufanya kitu km walikuwepo, unalinganisha na kuwekewa vikwazo ndio watokee..? r you insane!
 
vyombo gani..kwani 29/10 hadi 03/11 havikuwepo..? hivi tukio la kuua watu hawakufanya kitu km walikuwepo, unalinganisha na kuwekewa vikwazo ndio watokee..? r you insane!

Tuendelee kuzidisha visomo vyetu ili parapanda ilie na bendera nusu mlingoti iweze kupandishwa mapema kabla Mwaka huu haujaisha

Kapora uchaguzi na uhai wa Ndugu zetu na mbaya zaidi kawafukia kibabe
 
Wanastuka sasa? wakati kwenye akaunti zao za benki kuna mamilioni
 
haya mawazo yako ya kujikomba ndio utumwa unaopaswa kupigwa vita..unaposema huwezi kuukata mkono unaokulisha hali unajua mishahara,posho na marupurupu wanalipwa kwa mujibu wa sheria hivyo hata kiongozi au utawala ukibadilika wataendelea kulipwa vizuri sababu ni wajibu kisheria..japo pia nakubaliana wewe kwa aina ya viongozi tulionao wenye viburi,ubinafsi,roho mbaya na kukomoana na wasiojali sheria,haki na taratibu wanaweza kuamuru usilipwe hata mia na zaidi watakunyang'anya hata kidogo unachomiliki na kuwekeza wakakurudisha mavumbini..hii haina kujaribu kwani kama kuwatoa hao viongozi wabovu uwe mshindo moja tu ukifeli utaumia wewe
 
Samuya hana historia ya kuwa good academically, unategemea asiwe anafanya mambo ya kijinga?
 
Mnalialia nini sasa tulieni si mlitaka yote na barua mkawaandikia....


Kimyaaaaa
 
Tuendelee kuzidisha visomo vyetu ili parapanda ilie na bendera nusu mlingoti iweze kupandishwa mapema kabla Mwaka huu haujaisha

Kapora uchaguzi na uhai wa Ndugu zetu na mbaya zaidi kawafukia kibabe
..acha kujitoa ufahamu bwn, kwa sasa ishu iko mikononi mwa wananchi wenyewe kujipambania dhidi ya hivyo vyombo unavitaja, wao wanalinda mtu mmoja na genge lake..unawataja taja wa nini, hatutaki hata kuwasikia!
 
Kumbuka usaili wa kujiunga na jeshi ni kunywnyua matofali wala siyo akili.

Sasa ndugu mleta mada, unategemea mnyanyua matofali atafanya cha maana kama Traore??
 
..asee, una kazi na majini yako, wewe ukipewa oda na shetani kula mavi utakula..? hao vyombo uliowataja mwanzo hiyo ndio ajenda umeanza nayo, hatutaki kuwasikia! acha kujibaraguza..1
 
Yaani kweli Tanzania ni ndogo kuliko mtu Mmoja, yaani wananchi Milioni 70 tunaenda kuingia matatizoni kwa sababu ya mtu Mmoja???
..badilisha hiyo heading..lbd km unamaanisha vyombo ni vile vyombo vya jikoni!
 
Tena mtu mwenyewe ni kutoka nchi jirani
 
Very sad. Yaani Tanzania tunafikishwa huku kwa sababu ya mtu Mmoja na hapo akisafiri kwenda nchi yeyote iliyosaini Mkataba wa ICC watamdaka na kumpeleka ICC na hiyo Haki ataipata huko huko Gerezani akiwa ndani
Badly ICC hawana uwezo wa kumkamata akiwa president
 
Katiba ya ccm ya mwaka 1977 haimpi nafasi mteule wa Rais kumgeuka bosi wake hata akufanya madudu ya aina gani. Labda itokee tu awe mzalendo na hivyo aamue kujilipua kusimama upande wa haki au aangalie maslahi ya nchi! Badala ya maslahi ccm na Rais wa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…