Walah tungeathirika leo endapo tungepoteza hazina hii!!!!


Umenena kwa kweli. Huu uzin uwe ni wahsusi wa wanaume
 
Contact zake????For what??

kunauwezekano akapata coverage ili uwe mfano wa kuigwa ili na wale wakina mama wanaoshinda ndani wakipaka hina wajue umuhimu wa nafasi zao. jambo kama hili kama unaweza kuli-complement humtia moyo muhusika napia huwavutia na kuwafunza wengine. hope nimesomeka
 
Kuna watu huwa wanabahati ya mtende, chochote wafanyacho huwa na mafanikio tu hata kama hawajui madarasa, (huyu mama ni mmoja wao) pia kuna baadhi ya jamii ujasiliamali kwao ni asili, hufanikiwa bila elimu ya darasani, mfano; wahindi, wachaga, waha, machinga, n.k. Maisha hayana fomula wala ujanja ni kudra tu za Mwenyezi Mungu.
 

Una umri gani?Naona mwandiko kama wa kabinti vile!
 

Hivi bahati ni kitu gani????
 

Samahani Mkuu HorsePower. kusema cha ukweli nashikwa na kigugumizi kukubaliana na wewe.
Hivi hujui kwamba kuna kundi kubwa la wasomi tena wenye kiwango kikubwa cha elimu lakini wanatapeliwa kirahisi sana na wale wataalamu wanaojiita maprofesa wa aina ya MAJI MAREFU, ambao hata elimu yao ya msingi ni ya mashaka matupu.
Kuna waganga wengi sana wa asili ambao chumo lao kwa kiasi kikubwa linawategemea hawa tunaowaita wasomi. Zamani kidogo wateja wakubwa wa wataalamu hawa walikuwa ni sisi kina yakhe ambao hatumudu gharama za hospitali zaidi ya kupungwa maruhani, lakini kutokana na wasomi wengi kuwakimbilia wataalamu hawa ambao hata hivyo wengi ni matapeli, gharama za wataalamu hawa zimekuwa kubwa kiasi cha kutisha.
Zamani kidogo ilikuwa kumuona mtaalamu kama ndugu yangu MziziMkavu ilikuwa ni shilingi 50, lakini siku hizi bila mwekundu wa msimbazi hujapigiwa ramli.......LOL

nakubaliana na Eiyer, siku hizi wanaume na hata wanawake wanachagua wenza wao kwa kuangalia kiwango cha elimu au kazi aliyo nayo mtu (kwa upande wa kazi walengwa wakubwa ni wanaume). Utakuta msichana anamtambulisha mpenzi wake kwa mashostito wake, baadae mwanaume akiondoka au wakikutana siku nyingine ataulizwa... "Shosti hivi shem anafanya kazi gani....?"
Ole wake aseme ni mbangaizaji, watamnanga na kumkatisha tamaa, watamdhihaki eti ana mchumba mwenye kasoro, kisa hana ajira........!
 
Last edited by a moderator:
Mtaftaji bana................................LOL
 
Last edited by a moderator:
Kwa sababu wewe bado ni kula kulala, naamini ukikua utayaona
 

nilisoma kitabu kimoja," kiongozi aliye uchi". mke na mume walikuwa wanakwenda likizo kutoka huko anakofanya kazi mume, gari ikaisha mafuta wakaingia kwenye kituo cha mafuta kuongeza wese. hapo kukawa na jamaa mmoja amechoka ile mbaya ni mjaza upepo kwa magari ya watu pale kituoni. mke wa jamaa akawa anamwangalia sana yule mjaza upepo. wakiwa wameanza safari , bwana akauliza bibi" mbona ulikuwa unaangalia sana yule baba". bibi akajibu, yule ni boyfriend wangu wa kwanza , ndo alitaka kunioa kabla yako", bwaba akauliza tena, so umekumbuka mambo yake?, ungeoana nae basi tena leo ungekuwa bibi wa mjaza upepo". bibi akajibu, "hapana sikumbuki chochote , isipokuwa ninajiuliza nisingekukubali wewe manake leo ungekuwa mjaza upepo na si meneja kama hivi sasa"
 
Huu ni mfano mzuri wa kuigwa!
 
Haswa, mahala popote ukikuta kuna maendeleo ujue kuna maelewano mazuri na hasa kwenye swala la kipato. Jamani wanaume wamekua si wawazi kwny swala la kipat na ndo hapo unakuta maendeleo ni ya kusuasua.. pia mi huwa naamini mwanamke siku zote huwa anapenda maendeleo ya familia na mara nyingi si wafujaji wa pesa, then kwa kumshirikisha kuhusu kipato na mkapanga mambo ya kufanya siku zote mtafanikiwa.....
 

Suala la kushirikiana kwenye ndoa ni tatizo la kila upande!
 
kabla ya chochote binaadamu huzaliwa akiwa na akili na huzitumia akili hizo kuyakabili mambo mbalimbali yanayomzunguka,nasisitiza hutumia akili na si kitu kingine.elimu huja kuongeza maarifa katika akili zile na kumwongezea binaadamu werevu.sasa hii tabia sijui ya kuiga ya kuabudu elimu imewakosesha sana watu fursa,mume hakujali kwamba mkewe hajasoma alichojali ni kwamba mkewe ana akili na kupitia hizo akili mke akafanya mambo.sisi tulio wengi mama zetu hawakusoma lakini ndio mama bora kuliko hawa wamama wa kizazi cha sa sasa.akili na fursa ndio mpango mzima akiwepo na mungu hapo hakiaribiki kitu hapo.
 
DUU mke wangu ana digrii hata kuku hajui kufuga!lol!wanawake wa dot com tabu tupu wapo busy na facebook


we....unajua kufuga ata bata?

au una kipi kipaj like juu apo?

asi ndo nyinyi ata kununua kiwanja amtak.....fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…