Walah tungeathirika leo endapo tungepoteza hazina hii!!!!

Walah tungeathirika leo endapo tungepoteza hazina hii!!!!

huyo mama kafika hapo si tu kwa juhudi zake binafsi bali pia kwa sababu ya mume mwelewa aliye nae....
tena hii wanaume waichukulie kama changamoto, wanaume wangapi ambao wana mali hawataki wake zao wajue?
wanaume wangapi ambao mnawaficha wake zenu kipato?
wanaume wangapi ambao mna akaunti a siri?
wanaume wangapi ambao mnaachisha wake zenu kazi kwa ajili ya inferiority zenu au wivu usiokuwa na maana?
wanaume wangapi wanaokubali wake zao kujishughulisha? unakuta wanaume wengine mke kaanzisha kibiashara kikikua wateja wakija asiwachangamkie(hususan wa kiume)

familia inayoshirikiana na kufanya kazi pamoja ndiyo inayofanikiwa......

Umenena kwa kweli. Huu uzin uwe ni wahsusi wa wanaume
 
Contact zake????For what??

kunauwezekano akapata coverage ili uwe mfano wa kuigwa ili na wale wakina mama wanaoshinda ndani wakipaka hina wajue umuhimu wa nafasi zao. jambo kama hili kama unaweza kuli-complement humtia moyo muhusika napia huwavutia na kuwafunza wengine. hope nimesomeka
 
Kuna watu huwa wanabahati ya mtende, chochote wafanyacho huwa na mafanikio tu hata kama hawajui madarasa, (huyu mama ni mmoja wao) pia kuna baadhi ya jamii ujasiliamali kwao ni asili, hufanikiwa bila elimu ya darasani, mfano; wahindi, wachaga, waha, machinga, n.k. Maisha hayana fomula wala ujanja ni kudra tu za Mwenyezi Mungu.
 
sasa ulitegemea wasijitunze kwa usasa jukumu lk nn ww suruali?necha ya mama ni u rembo,ndo nyie mnaotaka wake zenu wawe km ma house girl wenu.ht mkitoka ham mech,unanukia casablanka mkeo ananuka kikwapa cha moshi wa kuni,wapi mmepotea c dunia ya sasa saloon km kawa ni jukumu lk kuhudumia mavazi,malazi na mahitaji mengine lau umeshindwa kaa ndani ukune nazi yy akatafute.

Una umri gani?Naona mwandiko kama wa kabinti vile!
 
Kuna watu huwa wanabahati ya mtende, chochote wafanyacho huwa na mafanikio tu hata kama hawajui madarasa, (huyu mama ni mmoja wao) pia kuna baadhi ya jamii ujasiliamali kwao ni asili, hufanikiwa bila elimu ya darasani, mfano; wahindi, wachaga, waha, machinga, n.k. Maisha hayana fomula wala ujanja ni kudra tu za Mwenyezi Mungu.

Hivi bahati ni kitu gani????
 
Eiyer utakuwa haukunielewa vizuri, sikusema kuwa elimu ndiyo inayoleta mafanikio ya biashara bali nilisema kuwa elimu ingemsaidia zaidi kupanua na kucontrol zaidi biashara yake. Elimu pia husaidia kumpanua mtu mawazo na pengine hata kuifanya biashara yake kuwa ya kimataifa. Na zaidi ya hapo, elimu inaweza kusaidia kupunguza kuibiwa kwa kutumia kalamu na kuingia kwenye mikataba hatarishi.
Hiyo mifano uliyoitoa ya watu wasiojua kusoma na kuandika, nakubaliana na wewe kuwa wapo na hata mimi nimekutana nao. Ila wao ni wazi kuwa walipata bahati ya kuwa na wasimamizi wazuri na waaminifu.
Hata hivyo nakubaliana na wewe na nilisema mwanzo kuwa si vyema tukawabagua wenzi wetu kwa sababu ya weakness fulani kama elimu, bali tuwatie moyo kuondoka na weakness hiyo kama kuna ulazima wa kufanya hivyo.

Samahani Mkuu HorsePower. kusema cha ukweli nashikwa na kigugumizi kukubaliana na wewe.
Hivi hujui kwamba kuna kundi kubwa la wasomi tena wenye kiwango kikubwa cha elimu lakini wanatapeliwa kirahisi sana na wale wataalamu wanaojiita maprofesa wa aina ya MAJI MAREFU, ambao hata elimu yao ya msingi ni ya mashaka matupu.
Kuna waganga wengi sana wa asili ambao chumo lao kwa kiasi kikubwa linawategemea hawa tunaowaita wasomi. Zamani kidogo wateja wakubwa wa wataalamu hawa walikuwa ni sisi kina yakhe ambao hatumudu gharama za hospitali zaidi ya kupungwa maruhani, lakini kutokana na wasomi wengi kuwakimbilia wataalamu hawa ambao hata hivyo wengi ni matapeli, gharama za wataalamu hawa zimekuwa kubwa kiasi cha kutisha.
Zamani kidogo ilikuwa kumuona mtaalamu kama ndugu yangu MziziMkavu ilikuwa ni shilingi 50, lakini siku hizi bila mwekundu wa msimbazi hujapigiwa ramli.......LOL

nakubaliana na Eiyer, siku hizi wanaume na hata wanawake wanachagua wenza wao kwa kuangalia kiwango cha elimu au kazi aliyo nayo mtu (kwa upande wa kazi walengwa wakubwa ni wanaume). Utakuta msichana anamtambulisha mpenzi wake kwa mashostito wake, baadae mwanaume akiondoka au wakikutana siku nyingine ataulizwa... "Shosti hivi shem anafanya kazi gani....?"
Ole wake aseme ni mbangaizaji, watamnanga na kumkatisha tamaa, watamdhihaki eti ana mchumba mwenye kasoro, kisa hana ajira........!
 
Last edited by a moderator:
sasa ulitegemea wasijitunze kwa usasa jukumu lk nn ww suruali?necha ya mama ni u rembo,ndo nyie mnaotaka wake zenu wawe km ma house girl wenu.ht mkitoka ham mech,unanukia casablanka mkeo ananuka kikwapa cha moshi wa kuni,wapi mmepotea c dunia ya sasa saloon km kawa ni jukumu lk kuhudumia mavazi,malazi na mahitaji mengine lau umeshindwa kaa ndani ukune nazi yy akatafute.
Mtaftaji bana................................LOL
 
Last edited by a moderator:
sasa ulitegemea wasijitunze kwa usasa jukumu lk nn ww suruali?necha ya mama ni u rembo,ndo nyie mnaotaka wake zenu wawe km ma house girl wenu.ht mkitoka ham mech,unanukia casablanka mkeo ananuka kikwapa cha moshi wa kuni,wapi mmepotea c dunia ya sasa saloon km kawa ni jukumu lk kuhudumia mavazi,malazi na mahitaji mengine lau umeshindwa kaa ndani ukune nazi yy akatafute.
Kwa sababu wewe bado ni kula kulala, naamini ukikua utayaona
 
Huyu mama ni mama wa watoto wa4,mwanae wa mwisho amemaliza chuo mwaka juzi na ameanzisha mradi wake wa kuku wa mayai.Mume wa mama huyu alistaafu kazi mwaka 2007.Lakini maisha yake hayajabadilika kutokana na miradi ya familia iliyoanzishwa na mkewe.Mama huyu hakuwahi kusoma utotoni,hii inamaana wakati anaoelewa na mumewe alikua hajui kusoma wala kuandika.Ni mwaka 92 ndipo alipojifunza kusoma na kuandika na alikua na umri wa miaka 35!

Aliolewa akiwa na miaka 14! Mumewe mama hupenda kumuita huyu mama kiongozi,humuita hivyo kutokana na mama huyu huwa kiongozi hasa. Mumewe mama huyu anasema,"maduka yote matatu,mashamba ya mpunga kule Bariadi,nyuma tano tulizopangisha pamoja na dispensary vyote ni mawazo na usimamizi wa mke wangu.Unajua wakati nafanya kazi sikua napata muda wa kutulia,nilipokua narud nyumbani kutoka safari mke wangu alikua ananiweka kitako na kuniuliza kama kuna hela nimeibakisha kutokana na malipo ya safari ofisini baada ya matumizi safarini,na nilipofanya ubishi alikua mkali kwelikweli.

Kutokana na mabaki hayo ya safari na akiba ya mshahara ambayo yeye ndo alilazimisha iwepo aliweza kufanya hayo niliyokueleza,na pia ameanzisha mradi wa kuwasaidia akina mama wenzake kwa kujikwamua kiuchumi kwa kuwakopesha pesa,anasema ndoto zake ni kuja kuanzisha benki".Hayo ni baadhi tu ya ushuhuda wa anayoyafanya mwanamama huyu ambae kafanya mazuri na hakuwahi kwenda shule tofauti na kujifunza kusoma na kuandika tena ukubwani.Hivi ingekua leo mama huyu angeolewa?Kwa jinsi tunavyopimana kwa elimu,rangi na pesa sidhani kama kuna kijana yoyote anaweza kuwa na mke/mume wa aina hii.Tunadhani elimu ndo inamfanya yoyote awe na ubinadamu tunaishia kujuta maishani,sisemi watu wasisome au shule haina maana,hapana,ila kuamini kwamba ukishasoma,au ukawa na hela haimaanishi una uelewa wa yote.

Au ukioa/olewa na "msomi" basi ndoa yako itakua na furaha na mafanikio la hasha.Huyu mama amekua msaada kwa familia yake na jamii inayomzunguka,ingekua leo si angeonekana sio binadamu na hastahili kuolewa na msomi kama mumewe?Binadamu wote ni binadamu,vitu vya nje haviwezi kubadili ukweli huu!

nilisoma kitabu kimoja," kiongozi aliye uchi". mke na mume walikuwa wanakwenda likizo kutoka huko anakofanya kazi mume, gari ikaisha mafuta wakaingia kwenye kituo cha mafuta kuongeza wese. hapo kukawa na jamaa mmoja amechoka ile mbaya ni mjaza upepo kwa magari ya watu pale kituoni. mke wa jamaa akawa anamwangalia sana yule mjaza upepo. wakiwa wameanza safari , bwana akauliza bibi" mbona ulikuwa unaangalia sana yule baba". bibi akajibu, yule ni boyfriend wangu wa kwanza , ndo alitaka kunioa kabla yako", bwaba akauliza tena, so umekumbuka mambo yake?, ungeoana nae basi tena leo ungekuwa bibi wa mjaza upepo". bibi akajibu, "hapana sikumbuki chochote , isipokuwa ninajiuliza nisingekukubali wewe manake leo ungekuwa mjaza upepo na si meneja kama hivi sasa"
 
huyo mama kafika hapo si tu kwa juhudi zake binafsi bali pia kwa sababu ya mume mwelewa aliye nae....
tena hii wanaume waichukulie kama changamoto, wanaume wangapi ambao wana mali hawataki wake zao wajue?
wanaume wangapi ambao mnawaficha wake zenu kipato?
wanaume wangapi ambao mna akaunti a siri?
wanaume wangapi ambao mnaachisha wake zenu kazi kwa ajili ya inferiority zenu au wivu usiokuwa na maana?
wanaume wangapi wanaokubali wake zao kujishughulisha? unakuta wanaume wengine mke kaanzisha kibiashara kikikua wateja wakija asiwachangamkie(hususan wa kiume)

familia inayoshirikiana na kufanya kazi pamoja ndiyo inayofanikiwa......
Haswa, mahala popote ukikuta kuna maendeleo ujue kuna maelewano mazuri na hasa kwenye swala la kipato. Jamani wanaume wamekua si wawazi kwny swala la kipat na ndo hapo unakuta maendeleo ni ya kusuasua.. pia mi huwa naamini mwanamke siku zote huwa anapenda maendeleo ya familia na mara nyingi si wafujaji wa pesa, then kwa kumshirikisha kuhusu kipato na mkapanga mambo ya kufanya siku zote mtafanikiwa.....
 
Suala la kushirikiana kwenye ndoa ni tatizo la kila upande!
 
kabla ya chochote binaadamu huzaliwa akiwa na akili na huzitumia akili hizo kuyakabili mambo mbalimbali yanayomzunguka,nasisitiza hutumia akili na si kitu kingine.elimu huja kuongeza maarifa katika akili zile na kumwongezea binaadamu werevu.sasa hii tabia sijui ya kuiga ya kuabudu elimu imewakosesha sana watu fursa,mume hakujali kwamba mkewe hajasoma alichojali ni kwamba mkewe ana akili na kupitia hizo akili mke akafanya mambo.sisi tulio wengi mama zetu hawakusoma lakini ndio mama bora kuliko hawa wamama wa kizazi cha sa sasa.akili na fursa ndio mpango mzima akiwepo na mungu hapo hakiaribiki kitu hapo.
 
DUU mke wangu ana digrii hata kuku hajui kufuga!lol!wanawake wa dot com tabu tupu wapo busy na facebook

we....unajua kufuga ata bata?

au una kipi kipaj like juu apo?

asi ndo nyinyi ata kununua kiwanja amtak.....fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Back
Top Bottom