Walahi ipo siku PCB itamuacha utupu huyu dogo.

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
11,492
Reaction score
5,047
JF...!
Wapendwa wana JF wadau wa elimu, nimechukua fursa kuomba msaada wa ushauri wenu kwa huyu dogo mwanaJF mwenzetu ambaye ni jirani yangu hapa home napoishi.

Dogo matokeo yake ya kwanza alikuwa na D's ktk masomo 6 (Hist, CIV, Chem, , Geo, Kisw, Lang) Pamoja na F za (Math, Phy na Bios)
div4-29

Mungu si Athuman baada ya uchakataji dogo akapata credit 4 za Chem, Hist, lang, Civ,
Pia na yale masomo mengine yote ya sayansi aliyopiga F hivi sasa kapata D yote. Div3-24

Kasheshe imekuja baada ya kupata matokeo mapya mazuri hivi sasa anataka asome PCB kisa kwao wazazi wamemwambia wanapenda asome sayansi ili aje kuwa daktari, Nimejaribu kumshauri asomee anachokiweza dogo kanitusi na kejeli,

Nimekuja hapa may be atawaelewa ninyi mkishauri maana ni member humu so ushauri wenu kwake ni wa muhimu sana.

Ahsanteni.
 
Mwaka huu walimu wa A-level wajiandae kufundisha vilaza, natumai matokeo ya form 6 ya mwaka 2016 itabidi tena tume ikae ifanye standadization la sivo vyuo vikuu vitakosa wanafunzi
 
Mwaka huu walimu wa A-level wajiandae kufundisha vilaza, natumai matokeo ya form 6 ya mwaka 2016 itabidi tena tume ikae ifanye standadization la sivo vyuo vikuu vitakosa wanafunzi

Mkuu itakuwa ni funga kazi, kibaya zaidi ya matokeo mapya yamewapata vichwa baadhi ya wanafunzi kuwa waweza sana na adui yao ni NECTA tu kwamba inawafelisha.
 
Duuh hy dogo ataumia kwn h comb nyingine sio za.kuiga eti fulani kwa vp anasoma comb hy na mm nisome. Anyway mtoto.akilia wembe mpeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…