Walaji wa kitimoto tujuzane kijiwe kipi kizuri kwa hapo ulipo

Walaji wa kitimoto tujuzane kijiwe kipi kizuri kwa hapo ulipo

DODOMA ...KWA MASISTA UASKOFUNI NI BALAA!
afu kwa Wale wanaopenda ile inayotengenezwa kwenye Vibanda umiza😀Pale Mkabala na RC NKUHUNGU Kama unaanza kuelekea Chang'ombe kuna Kina Manka Kibao na wamekubuhu katika maandalizi ya hii haramu.
Pia Mkabala na Bunge kule kwenye Vibanda vya Mama Nchimbi kuna Bar sio nzuri kivile lakini wanatengeneza kitu inachanganywa na mchicha ni hatari!
I see nilipita hapo mwezi Aprili, wana kitimoto ya kuchoma iliyotulia aana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wa tanga chimbo gani jingine zuri nishawah kupita sabasaba ila kitimoto chao sijawah kukipenda
 
Bar ya Majumba ya Mawe Msamvu morogoro nyuma ya sheli ya puma extremely amazing ndio nakula kabla sijaunga dodoma hadi sausage za mnyama unapata hadi kitichoma ipo, kuku na beef pia

Tujuzane kijiwe kipi kizuri kwa hapo ulipo kinapika kitimoto chenye Quality yaani ukigusa utatamani kesho uje tena?

Kama mnavyojua Utamu wa kitimoto upate na ugari au Ndizi za kukaanga,nimeshapanga ratiba yangu leo lazima nikale kitimoto.

View attachment 942375

View attachment 942377

Nb:
Mashekhe na Maustadhi tafadharini sana msije kuutia shombo uzi huu,

Huu ni kwa sisi wala kitimoto tu ukiona haukufai kafanye mengine siyo kuja hapa.


Cc Zero IQ
 
Kilimanjaro (Boma) - Barabara ya kwenda Lawate, upande wa kushoto kuna Bar ndogo ndogo ina hii huduma.

Kilimanjaro (Mtaa wa Karanga opposite Magereza) - Kuna fundi mmoja yuko mwisho kabisa wa zile frame za biashara. Ana balaa huyu jamaa. Anatoa kitu safiii sana.

Mbeya (mjini) - Penge restaurant maeneo ya Mzumbe Uni.

Mbeya (mjini) - Barabara ya kwenda hotel za Mfikemo kuna vibanda vingiii.

Mbeya (mjini) - Chini ya Chaula Pub karibu kabisa na chuo cha mzumbe.

Arusha - Kimandolu eneo la Njia ya Ng'ombe pale kuna mtaalam kajiwekea kibanda safii.

Arusha - Mianzini mkabala na CRDb office kuna vibanda vingii.

Arusha - Mwanzo wa Barabara ya kanisa la Father babu ukitokea ALMC hospital.. karibu na mafundi wa furniture wameweka vitanda nje na makabati. Kuna Bar siijui jina. Wako vizuri sana.

Arusha - Karibu na mahakama ya Wilaya kuna bar inaitwa Apache. Huduma safi na salama.View attachment 1413668

Sent using Jamii Forums mobile app

aah iyo ya mbeya chini ya kwa chaula ni balaaa yaani


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisa? Mi nilienda mara moja tu sikurudi tena

Mibbs ni overrated hamna kitu



Sent using Jamii Forums mobile app

Nilienda saa 7 mpaka saa 10 sijaletewa chakula na nilikua mjamzito njaa iliuma mpaka nikataka kuzimia mbele naona giza, nawaambia wahudumu najisikia vibaya sana nileteeni wanajizungusha tu nikaishia kupelekwa Marie Stopes.

Toka hapo sijaenda na kila nnaekutana nae akitaka kwenda namshawishi asiende.
 
Back
Top Bottom