CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,872
- 9,263
Habari za Mwaka mpya wakuu,
Mwaka mpya nazani ndo umeanza wakuu na uko speed sana.
Kuna maswala ya muhimu sana ya kuyafanyia kazi kama Watanzania na kama wajasirimali.
1. ISHU YA UJASIRIMALI
Kwa kweli tuna kazi moja ngumu sana katika swala zima la ujasiriamali, tunatakiwa kukimbia wakati wenztu wanatembea wenzetu wako very far na that is why so far wanaelekea kututawala, Ishu ya Kenya kuwa mwekezaji No mbili Tanzania si ishu ya kufurahia hata kidogo ni fedheha ya hali ya juu kabisa, kwa nini sisi tusiwe wawekezaji wakubwa Kenya?
Last year nilkuwa na safari ndefu sana huko kenya ambayo ilinichukua kwenye kufika kwenye miji mikubwa karibia yote ya kenya kama vile KISUMU, ELDORET, NAIROBI, NAIVASHA sikufika tu MOMBASA.
Katika miji hii yote na wengine walio fika huko ni mashahidi.
1. Sikuweza kuona bidhaa ya Tanzania hata moja.
2. Maduka yote yamejaa bidhaa za kenya tupu.
3. Hata pombe wanakunywa za kwao Tusker Lager kusapoti kiwanda chao,huwezi wakuta wanakunywa sijui Serengeti,
Ila kwa Tanzania ni kinyume chake hata ukienda Mtwara au Mbeya utakuta bidhaa za Kenya.
Huwezi kuta bidhaa za Tanzania hata kwenye miji inayo pakana na Tanzania, sikuwezo ona kabisa.
UFUGAJI WA KUKU KENYA.
Kenya wako mbali sana Africa mashariki na kati kwa ufugaji wa kuku na hii si kwa bahati mbaya bali jamaa wana mikakati ya hali ya juu kabisa kabisa, jamaa wamejpanga vilivyo na hawana utani kabisa, na moja ya sababu kubwa kwa nini kenya wako juu sana kwenye kuku ni kwamba.
1. Kenya wana kula sana kuku kuliko Tanzania, hii haina ubishi, wakati sisi ni nyama nyekundu Kenya wanakula sana white meet ya kuku. ukitembelea migahawa yao mingi ni kuku watu wanaagiza tofauti na Tanzania ambapo sisi kuku ni kwa bahati mbaya tu. hii ndo moja ya sababu
Na Kuku jogoo ambaye kwenye anauzwa hadi Tsh 30,000/ huku kwetu utaambiwa Tsh 15,000/
BIASHARA YA SUPERMARKET na ISHU YA NAKUMAT KUCHUKUA SHOPRITE.
Hawa jamaa ni kweli kwamba wana Malls nyingi sana na hii ni kwa sababu wana utamaduni wa kununua vitu supermarket, nui vigumu sana miji mingi ya kenya hasa mikubwa kukuta maduka ya rejareja, ni machache sana, Mji kama Kisumu unaweza zunguka mji mzima ukakutana na maduka matano tu ya bidhaa za reja reja, haza za kula tofauti na maduka ya simu na kazalika ambayo ni kama huku tu.
Hii inawapa advantage na hata NAKUMAT anavyo chukua maduka ya Shoprite si kwa bahati mbaya jamaa wana nguvu sana huko kwao na si zani kama kuna Supermarket ya kuweza kushindana nao hapa Tanzania,
UZALENDO
Jamaa nao wanatuzidi sana kwenye swala la uzalendo, wanapenda sana vitu vy nchi yao, wanapenda sana nchi yao, ni vigumu kukuta wakenya sijui wamevaa urembo una rangi za bendera za USA tofauti na sisi mtu anatundika Bendera ya USA anazani ni ujanja kumbe ni ujnga wa hali ya juu kabisa,
Hata TV huwezi wakuta sijui wanatazama TV za Bongo Na hata EATV sijui kwa nini wanaitwa hivyo make hakuna mtu anatazama hiyo TV na hata hawaijui,
NINI TUFANYE?
1. UZALENDO
Ni lazima kwanza Watanzania wawe wazalendo na vitu vyao, wajivunie vitu vyao hata kama ni vibaya kiasi gani, china alianza hivyo hivyo, tunatakiwa kupenda vya kwetu, na si kupenda vya wengine tunazani sifa wakati wao hawapendi vya kwetu.
2. UJASIRIMALI KWA UJUMLA WAKE
Tunatakiwa kufanya kazi kufa na kupona, kama wewe ni mjasirimali basi pambana kufa na kupona, Ujasirimali si lele mama, si showoff, watu wanachukulia kama sifa fulani lakini sio hivyo tunatakiwa kujitoa viulivyo ili tuweze kufanikiwa.
- TUWE WABUNIFU
Ubunifu ndo kitu kitaweza kutuokoa, ni lazima tuwe wabunifu la sivyo ni hakuna kitu, wenzetu ndo kitu kinawasaidia,
MFANO: WEWE UNAFUGA KUKU. Je ulisha jiuliza utaongezaje walaji wa Kuku ili basi upate soko? au unawaza kuuza tu?
Tuache kujikita kwenye sales pekee,sales ni ishu ya muda tu ni lazima tujikite kutengeneza soko na si kujikita kuuza tu,
3. TUACHE MANENO MENGI NA VITENDO 0
Tunapenda sana maneno, Watanzania tunafanya biashara za maneno, huku janvini kwenyewe ni mfano tosha, tuko kw amaneno tu lakini kiuharisia hakuna kitu,
Watu wanapenda kutafuta sifa za kuja kusifiwa humu kwamba sijui wanafuga kuku, Nguruwe Bata na kazaila, wakuu tupige kazi sifa hazitatusaidia
Ni lazima vitendo vifanye kazi zaidi
4. MITANDAO
Ni lazima watu wajenge mitandao ya biashara na club za ujasiriamali, huku kila mtu naona yuko kivyake vyake, ok ni sawa but huwezi furukuta mbele ya wenzako, ni lazima wabongo tujenge hiyo mitandao
Wenzetu hutumia siku za wikendi kukutana na kubadilioshanaa mawazo huku wikenda tuna ulizana tukanywe wapi au wapi tukacheki mechi.
Ni lazima watu wafahamiane wasaidiane wajenge umoja ambao unaweza kutusaidia kusongo mbele na hata kupambna na competitors kutoka nje.
Ni lazima watu sasa wajenge mitandao/club na wawe wanakutana mara kwa mara tusipende kujifungia ndani wakati huko nje watu wanapiga kazi na wako mbali sana
5. TUPENDE KUINGIA GHARAMA KUFANYA TAFITI AU KUJIFUNZA KWA AJILI YA KUBORESHA BIASHARA ZETU.
-Tunapenda sana vitu vya Bure, mtu kahangaika katunga kitabu chake mtu anakitaka bure, tuache mambo ya bure, ili ufanikiwe ni lazima na wewe utoe pesa, Unakuta kuna semina za labda za kufuga kuku au Bata, mtu ana taka ahudhurie bure au aende and then alipwe, huu ni uwenda wazimu.
Ni lazima utafute taarifa au elimu ya biashara yako mahali kokote kule inako patikana kwa gharama yoyote ile, tusikae halafu mtu anakuja kupost huku kuuliza kama sabuni zina soko au la, huu ni ujinga,
Ni lazima uwekeze vya kutosha ili ufanikiwe ni lazima ugharamike, hakuna mafanikio ya bwerere.
6. TUWE SIRIASI
Watu hatuko siriasi, kuna post inaweza anzishwa ukaona kabisa kwamba hatuko siriasi hata kidogo,
If you dont build your dream, someone else will hire you to help them build theirs. Dhirubhai Ambani