Walaka wa I Kwa Wajasiriamali wote/Wafanya biashara/Wajasirimali watarajiwa

Walaka wa I Kwa Wajasiriamali wote/Wafanya biashara/Wajasirimali watarajiwa

Mleta mada asante sana, unachosema ndo ukweli, niko mwanza na hivi sasa nafanya kazi ya kuwaunganisha wajasiriamali hapa na ukanda huu.
 
Ni kweli ingeundwa club moja yenye matawi cos zikiundwa nyingi nyingine zitakosa nguvu na kama hazina link zitakufa lakini ikiwa moja na matawi tawi likikosa nguvu tawi la kanda nyingine linaweza kutuma wawakilishi na kazi au na bidhaa zao kuenda kutoa kitu kama hamasa na kuleta changamoto na hatimaye kuinua tawi hilo au mnasemaje wakuu
 
Ni kweli ingeundwa club moja yenye matawi cos zikiundwa nyingi nyingine zitakosa nguvu na kama hazina link zitakufa lakini ikiwa moja na matawi tawi likikosa nguvu tawi la kanda nyingine linaweza kutuma wawakilishi na kazi au na bidhaa zao kuenda kutoa kitu kama hamasa na kuleta changamoto na hatimaye kuinua tawi hilo au mnasemaje wakuu

Ni vigumu sana, kinacho takiwa ni watu kuwa na jumuia zao tena inatakiwa wale wenye product zinazo fanana, Kama ni wafuga Kuku basi wanakuwa na yakwao, kama ni Nguruwe hivyo hivyo, Kilimo hivyo hivyo, kama ni wauza mayai/wanunua mayai hivyo hivyo.

Kuwa moja nchi nzima ni ngumu sana, kinacho takiwa ni maeneo ya jirani, mwanza wanakuwa na ya kwao ambapo wao sasa wanaweza kuwa wana waalika wengine kutoka hata mbeya au Dar wanakuja kuwapa shule au kubadilishana uzoefu.

ya nchi inaugumu sana, hii nchi ni kubwa sana, ni vigumu sana kukutana, cha kutakiwa fanyeni za maeneo yenu, mnakuwa mnakutana wikendi badala ya kwenda kuangalia wanaume wakiingiza pesa uwanjani sisi tunakutana kujadili jinsi ya kuingiza pesa yetu.
 
Mleta mada asante sana, unachosema ndo ukweli, niko mwanza na hivi sasa nafanya kazi ya kuwaunganisha wajasiriamali hapa na ukanda huu.


Ila ili iwe na mafanikia ni lazima muwe wote mnafany kazi zinazo fanana, sasa mkukutana wengine wana miliki stationary, wengine, wanafuga kuku hapo hakutakuwa na kuelewana. Na ni vizuri zikahusu watu ambao tiyari walisha jitoa na si mtu anakuja anasema ana wazo lake, no wazo so ishu kinacho takiwa ni ionekane likifanyiwa kazi.

So Mkuu unaweza Mobilize na kwa kuanzia unaanza na wa mtaa wako na mnakuwa mnapanuka kidogo kigogo na mpaka mwaka uishe mnakuwa mmekamata mkoa mzima. haina haja kuanza na mkoa au mji mzima kwa wakati mmoja, No kidogo kidogo na mnaweka malengo kila baada ya muda fulani mnatakiwa muwe mmefikia watu kadhaa,

Na uzuri wa hii anaweza anza mmoja kuwakusanya watu na hata ukipata kumi ni hatua kubwa sana, na kutoka hapo mnaweza songa mbele, kinacho takiwa ni kuto kata tamaa mapema
 
Iwe club ya ujumla kisha kuwe na matawi kwa mikoa, hii itakuwa vyema sana, inawezakena hata kupanga safari ya kutembeleana kimkoa kujifunza. Mi nafikiri anzisha thread yenye conditions watu tujiunge halafu kila mtu aseme yuko wapi.

Mkuu nasisistiza inapendeza zikiwa hata nyingi kwa kila mkoa, Mfano kwa Arusha kunaweza kuwa na club/chama/jumuia au vyovyote vile za Wafuga kuku, wafuga ngo'ombe, wenye migahawa yao na kazalika, kutoka pale sasa mnaweza nyia wenye kufuga kuku mkawaalika wenye migahawa na mnajadiliana jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja, Tatizo wabongo tumelala sana na tutakuja kushituka kumekucha.
 
Uzi wako umenisaidia nilikuwa nimelala kimaendeleo ngoja niamke ili tupambane kuiweka nchi yetu kwenye ramani
 
Kinacho takiwa ni watu waache maneno, huu uwe mwaka wa Vitendo, ni lazima some time inapo fika mwisho wa mwaka ujiulize kwamba umepiga hatua gani? Je kuna cha maana umefanya? je kuna cha maana hata ukifa leo utaacha kumbukumbu kwa ndugu jamaa na hata familia yako?

Ni muhimu sana watu tukawa tunafanya tathimini ya yale tunayo fanya kila mwisho wa mwaka, kuliko kukaa kushamgilia mwaka mpya.

Tuache maneno tufanye kazi, Wabongo tunasifikla kwa maneno mengi sana na practise sifuri, Badala kila wikendi kupoteza musda sijui kwenda viwanja watu mnaweza tumia huo muda kukutana na kubadilishana uzoefu inapendeza sana, Viwanja vipo sana na vitaendelea kuwepo.

Tunaachwa nyuma sana na sisi tunabakia kulia na serikali, ni lazima tuamke, hatuwezi shindana na wachina wa kariakoo kwa maneno. Hatuwezi shindana na wenzetu wa EAC kwa maneno, kinacho takiwa ni vitendo tu, maneno hayajengi.

NI BORA KWAKWELI WATU WAKATENGENEZA MITANDAO YAO NA WAKAWA WANAKUTANA MARA KWA MARA KUONA WANAWEZA VIPI KUSONGA MBELE, NA MNAWEZA HATA MTAFUTA MTAALAMU HATA KAMA NI KUTOKA NJE YA NCHI AKAJA KUWAPA SHULE, Tuache kutumia muda mwingi kwenda sijui kutazama ligi ya Uingereza wale wako kazini, wanaingiza pesa
 
Mie nasema habu tuanze sisi wenyewe, wewe mjasilimali umyesoma huu uzi, je wajivunia bidhaa zako ama unahaha kuuza na kwenda kununua made in china, jeje nidhaa yako ina nembo gani? Made wapi???😕😕:thumbup:
 
Back
Top Bottom