Kinacho takiwa ni watu waache maneno, huu uwe mwaka wa Vitendo, ni lazima some time inapo fika mwisho wa mwaka ujiulize kwamba umepiga hatua gani? Je kuna cha maana umefanya? je kuna cha maana hata ukifa leo utaacha kumbukumbu kwa ndugu jamaa na hata familia yako?
Ni muhimu sana watu tukawa tunafanya tathimini ya yale tunayo fanya kila mwisho wa mwaka, kuliko kukaa kushamgilia mwaka mpya.
Tuache maneno tufanye kazi, Wabongo tunasifikla kwa maneno mengi sana na practise sifuri, Badala kila wikendi kupoteza musda sijui kwenda viwanja watu mnaweza tumia huo muda kukutana na kubadilishana uzoefu inapendeza sana, Viwanja vipo sana na vitaendelea kuwepo.
Tunaachwa nyuma sana na sisi tunabakia kulia na serikali, ni lazima tuamke, hatuwezi shindana na wachina wa kariakoo kwa maneno. Hatuwezi shindana na wenzetu wa EAC kwa maneno, kinacho takiwa ni vitendo tu, maneno hayajengi.
NI BORA KWAKWELI WATU WAKATENGENEZA MITANDAO YAO NA WAKAWA WANAKUTANA MARA KWA MARA KUONA WANAWEZA VIPI KUSONGA MBELE, NA MNAWEZA HATA MTAFUTA MTAALAMU HATA KAMA NI KUTOKA NJE YA NCHI AKAJA KUWAPA SHULE, Tuache kutumia muda mwingi kwenda sijui kutazama ligi ya Uingereza wale wako kazini, wanaingiza pesa