Wale ambao hatukuwahi kuwa wasafi siku ya ukaguzi shule ya msingi tukutane hapa

Wale ambao hatukuwahi kuwa wasafi siku ya ukaguzi shule ya msingi tukutane hapa

Deadbody

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Posts
4,274
Reaction score
6,595
WANAFUNZI+SHULE+YA+MSINGI+VITONGA+MVOMERO+PIX+NO+2.JPG


IMG_0038.JPG


Me nikikumbuka siku ya alhamisi kule shule ya Msingi kule Banana huwa nilikuwa nakerwa sana siku ambayo nimejitolewa kwenda mstarini (maana siendagi) halafu wale wapiga ngoma wanaanza kiherehere cha kupiga ule mdundo wa "Wachafu watoke mbele".Dah sikumbuki kama kuna siku niliwahi kuwa msafi na nimekamilika kuanzia tai ,nembo mpaka soksi.

Yani walimu walituzoea kutuona mda wa ngoma!

Kile kimdundo kilikuwa lazima kiondoke na mimi kwa makosa yafuatayo:
1.Mchafu(Nguo hazijafuliwa week)
2.Sina nembo ya shule
3.Sina tai
4.Viatu sio vyeusi
5.Viatu havina kamba
6.Nimevaa T-Shirt badala ya shati la shule
7.Kaptura ya zambarau badaya ya blue

Dah mikosi nilianza zamani!
 
Back
Top Bottom