Wale ambao hawajawahi kununuliwa zawadi na wapenzi/wake zao karibuni tufarijiane

vposterior

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2018
Posts
732
Reaction score
1,233
Habari zenu wanajamvi. Sijui ni mimi tu au wapo wenzangu ambao tangia waanze kuwa na mahusiano hawajawahi kununuliwa hata peremendi tu na wenza wao.

Mke wangu mimi ni house wife (though anajifundisha kazi za amali now) so simlaumu sana na yeye amewahi kuniambia anatamani kuninulia japo shati la mtumba ila lazima iwe ni kwa hela yake mwenyewe sio itakayotokana na mikono yangu.

Wale ambao hamjawahi kupewa kizawadi chochote mnajiskiaje?
 
Mkuu ilo ni tatizo kubwa sana hasa kwetu sisi wanaume, tunawapa wenzetu lkn wao sijui n ugumu hata sijui niiteje
 
Tena wengine wana kazi nzuri sana kipato Alhamdulillah lakini hata ile boksa hakuna.
 
Poleni sana wale wote ambao hamjawahi kupewa zawadi msife moyo ipo siku mtapewa.
 
Wanawake ambao MNA kiheherere kama mm tujuane, hivi mm nani aliniroga? Lakini mbona siaminigi uchawi? Sijui ni huruma ama? Yaani nikiingia mahusiano na mtu , cha kwanza naamza kuwaza ana body gani? Vip size yake ya viatu? Saa n.k hata kama Siku hiyo sina hela ila lazima niliweke kichwani, na mavazi yao sasa yalivyo gari. Yaan naonaga nisipompa kitu basi moyo unaumwa, ahaaaa jiulize sasa huwa napata nini in return.😁😁😁😁
Yaani ninavyopendaga zawadi jamani sijawahi pewa zawadi ila pesa napewa tena ndefu sio vielfu 30 vya watoto.

Naapaga kutotoa tena , nikiingia mahusiano, nikipita tu madukani narudia tena sijui nafel wapi? Ujinga gani huu? Aiiiii nimeacha kuanzia leo.

Haya na nyie wanawake mseme yenu nisijione mpweke mxeew nyau nyinyiπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kongole mkuu, wanawake wengine inabidi muige kwa Luckyline.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…