Wale ambao tunaishi na watoto wa watu na hatujapeleka hata 100 ya mahari tukutane huku

Wale ambao tunaishi na watoto wa watu na hatujapeleka hata 100 ya mahari tukutane huku

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Kusema ukweli huyu mwanamke ninaye ishi nae nilimchukulia kwa dada yake na kuamua kuanza maisha na yeye.

Basi bhana ilitokea msiba nyumbani kwao ikabidi tuende wote, na baada ya msiba kuisha ikabidi mambo mengine yaendelee ikiwepo kikao kuyahusu maisha yangu na yeye lakini kwa busara zao wakaniambia niende nikapambane siku nikipata kidogo niende nacho ili wakanitajie rasmi kiasi cha mahari.
 
kusema ukweli huyu mwanamke ninaye ishi nae nilimchukulia kwa dada yake na kuamua kuanza maisha na yeye basi bhana ilitokea msiba nyumbani kwao ikabidi tuende wote,
na baada ya msiba kuisha ikabidi mambo mengine yaendelee ikiwepo kikao kuyahusu maisha yangu na yeye
lakini kwa busara zao wakaniambia niende nikapambane siku nikipata kidogo niende nacho ili wakanitajie rasmi kiasi cha mahari,
Nimeipenda hii
 
Mahari ni tamaduni yetu pendwa
wala si utumwa
wala si kumnunua mwanamke

Mahari ni heshima kama zawadi iwa familia. Ya kukutunzia mke wako. .

Mahari haiko Africa tu, ipo kwenye jamii nyingi sana duniani. .

Lipa mahari Linda heshima ya mwanamke na familia yake. .
 
Lipa mahari Linda heshima ya mwanamke na familia yake. .
Kulipa mahari hii ya mara moja ni kuondoa heshima ya mwanamke na familia yake.

Mahari ni bei ya kumnunua mwanamke. Ukilipa mahari, unachosema ni kwamba huyu mwanamke thamani yake ni hii. Nalipa nimchukue. Umemfanya kawa kama ng'ombe.

Unaweza kulinda heshima ya mwanamke na familia yake kwa kukaa naye mpaka kifo kiwatenganishe.

Unaweza kulinda heshima ya mwanamke na familia yake kwa kuzaa naye mtoto.

Na kama material thing is your measure, unaweza kulinda heshima ya mwanamke na familia yake kwa kumpeleka shopping ambayo ni zaidi ya hiyo mahari kila mwezi.

Yani ni hivi, unakataa kulipa mahari mara moja, unalipa mahari kila mwezi kwa kuelewa umuhimu wa huyo mwanamke.

Akitaka dhahabu unambebesha mpaka anasema hizi nzito sana siwezi kuvaa wewe mwanamme utaniumiza. Yani dhahabu kubwa mpaka masikio yanataka kukatika, anaomba poo mwenyewe.

Akitaka nguo unamuachia mwenyewe achague anavyotaka.

Mahari hapo inakuwa endelevu, kama ilivyo ndoa.

Unajenga naye nyumba ya maana mnamiliki.

Unamnunulia latest cars, akiendesha anajisikia anamiliki barabara.

Yani bei ya BMW moja tu unalomnunulia ni mara 10 ya mahari unayoambiwa kulipa mara moja.

Ukitoa mahari mara moja unakuwa kama umemnunua ng'ombe.

Nikikupa mfumo huo wa mahari utauonaje?

Utauweza? Utaupenda?
 
Yani bei ya BMW moja tu unal9mnunulia ni mara 10 ya mahari unayoambiwa kulipa mara moja.

Ukitoa mahari mara moja unakuwa kama umemnunua ng'ombe.

Nikikupa mfumo huo wa mahari utauonaje?

Utauweza? Utaupenda?
Mahari ni Utamaduni ,ina maanisha usione vyaelea vilitunzwa mpaka unakutana nae, alizaliwa akalelewa alisomeshwa aliuguzwa alipoumwa akakua akasaidiwa aanze maisha Sasa wewe unakutana nae yupo ready na maisha labda kaanza kujitegemea na wewe tayari umeanza kujitegemea ni rahisi kusema mmependana muanze maisha pamoja.

Kwa tamaduni za Afrika mtahesabika nyie wahuni tu mmechukuana mnafanya uzinzi tu hamtapata baraka za wazazi ne je mtoto wa watu akikufia utamzika mwenyewe, akikuambia wazazi wake wanaumwa utaenda kuwaona wazazi wake wewe kama nani.

Jamii za watu wa Ulaya na America nyingi ndio hazina hizo mambo ya mahari sababu kubwa zimekomaa na maisha ya kibepari na Serikali zao zina pesa kusaidiana mahitaji binafsi ya watu sio lazima ndugu wahusike kwa Afrika tamaduni na Serikali hazijimudu kihivyo.

Tamaduni za kiafrika zinaishi kindugu, zinauguzana, zinasaidiana zinafurahi na kuhuzunika pamoja, harusi kwa Afrika ni jambo la kindugu na kijamii, mahari ni sehemu ya tamaduni za Afrika hata kama mmeona Ulaya peke yenu itawabidi mje Afrika kutimiza matakwa ya kitamaduni, hata makanisani mkitaka mjifungishe ndoa mtaulizwa kama mmemalizana na mambo ya tamaduni zenu kama mahari na wakati mwingine mahari sio lazima.

Pesa inaweza ambiwa lete blanket, lete mashuka leta ng'ombe, mbuzi au kuku unajua maana yake? Vijana wengi wa siku hizi wakitajiwa hivyo husema wapigiwe hesabu hivyo vitu shs ngapi, wazee wanaojua mila hukataa pesa hutaka kama blanket ulete blanket kwao blanket ni kumbukumbu ya kumuaga mtoto wait kuliko pesa ambayo watatumia itaisha na haitakuwa kumbukumbu nzuri ya kuagana na binti yao.
 
Back
Top Bottom