leo nimefurahi baaada ya kusoma hii post, mmenikumbusha hadithi za Fumbuka na kingereza chake, sasa hivi ni mkuu wa shule maeneo ya Kilwa huko,nilikutana nae Temeke sterio akinunua nguo, Kabahoza baada ya zile skendo za mapenzi na watoto wa shule alihamishiwa kwao bukoba, ila anaonekana sana Ukonga hasa nyakati za likizo, Libaba huyu alikua mwalimu wa historia kwa HGE alistaafu akawa mkulima kule Ruvu ila inadaiwa alipewa mkataba wa kazi kule Ruvu secondary.
nakumbuka miogo ya kisarawe, chapati za mama babu...daah masikini ananidai bill yake ya kama wiki mbili.
Hivi yule mwalimu wa kifaransa alikuaga anapiga picha alikua anaitwa nani?
kuna jamaa anaitwa Shikunzi John , huyu alimaliza HGE mwaka 2000, alikuaga anawakusanya madenti wa form twa hadi four kwa lengo la tuition ya bure, miaka mingi baadae kumbe nikaja gundua kumbe ilikua mbinu ya kupatia totozi,
wapo wasela wengine kama Tumaini kweka, SAMSON MWASAKAFYUKA ...Huyu alikua mzee wa shaban Robert dom kisha baadae Mnyapara.Bishoo Nelly Kamninyoge sasa hizi ni afisa uajiri serikalini. Juma samson Josluo sijui yuko wapi siku hizi.
Niungane na wengine wote kumuombea pumziko la amani Mjale P. MKUU WETU WA SHULE. ipo siku tutakutana tena maana nasikia kuna bonge na party linaandaliwa kwa wote walio maliza pale, nawambeni wale EGM, PCB, PCM NA HGE mliomaliza may 2000, tujitokeze tukumbuke mambo yetu.