wale tulio badilishwa mtazamo na wanawake tukutane hapa

wale tulio badilishwa mtazamo na wanawake tukutane hapa

Kuna mmoja alinihadithia alianza mpaka kwenda kanisani wakati alikua anajulikana mtukuti wa shule. Kupiga walimu kuwatukana kuchoma shule na kila kitu ila alivyomuona mwanamke anaempenda alikua boya akabadilika kabisa akawa sio yule gangster tena
 
Kuna mmoja alinihadithia alianza mpaka kwenda kanisani wakati alikua anajulikana mtukuti wa shule. Kupiga walimu kuwatukana kuchoma shule na kila kitu ila alivyomuona mwanamke anaempenda alikua boya akabadilika kabisa akawa sio yule gangster tena
asee hiyo ipo mkuu na asilimia kubwa ata kwene ndoa wanawake ndo huwa wanatubadilisha

unakuta adi unaacha gambe kwa ajili ya mwanamke
 
Hahaha, weka picha mkuu!..
habarini wakuu poleni na majukumu,kama heading inavosema

nakumbuka mwaka 2002 wakati nipo form three shule moja hivi iko iringa nilikua sipendi kabisa shule kwa mwezi nlikua nikionekana shule siku tatu basi ni mungu tu kasaidia,basi kipindi iko nilitokea kumpenda binti mmoja hivi alikua ni mrembo sana according to my blessed eyes alikua msafi adi anaboa, Asa si unajua mapenzi ya kitoto yalivo nlikua natamani kumuona kila dakika asa ntamuona vp na mi shule huwa sifiki ikanibidi nianze kwenda shule kila siku ili tu niuridhishe moyo wangu, mwisho wa siku adi utoro nikaacha nikawa mwanafunzi mwema



nilikua sipendi kabisa kusali isitoshe nilikua Muslim afu yeye alikua Catholic koo vipindi vikawa vinatofautiana ila kwa sababu nilikua nampenda sana kila mda na kua na hamu ya kumuona ikanibidi nianze kuingia Roman wenyewe walikua wakiitaTYSS Kama sikosei kila siku ya dini nilikua naingia ikafika stage nikabadili mpaka dini


nilikua mchafu sana kwangu huwezi tofautisha jumatatu na ijumaa lakini kwa sababu yake nikaanza kung'aa adi viatu nikawa na brush masela walinishangaa sana

nilikua kawaida sana kitaaluma nikaanza kusoma kwa bidii kwa sababu yake

NB:yote hayo nilikua nafanya nikidhani pengine ntafikiriwa na kua wake ila sikuwai kumuelezea hisia zangu adi kesho ila kwa kifupi yeye ndo alinibadilisha
 
Back
Top Bottom