Wale tulio wahi kuishi maisha ya machimboni tukutane hapa

Wale tulio wahi kuishi maisha ya machimboni tukutane hapa

Manyani wa katoro ni tishio wana roho ngumu balaa
 
Kwa upende wangu ni dhahabu, tusubir wa mererani watup maisha yao ,na wazee wa ruby na Vito vingine
Kwa mfano.ukitaka kuwa mchimbaji wa kujitegemea.alaf hauna hela ya kula machimboni,utaweza kweli?
 
Kama mashimo yanatema huwa kuna watu wanakuwa na hissa kwa kuwalisha msosi na vitu vya Ku bust energy mkitoa mzigo wanapata share
Duuh kama hamna mali iliyotoka?si mtalala njaa
 
Mgodini hujui majira yanaendaje kule hmna kusali kwamba Leo n jumapil ,jumamos wala ijumaa kila Siku n weekend na kila siku ni siku ya kazi
 
Mgodini hujui majira yanaendaje kule hmna kusali kwamba Leo n jumapil ,jumamos wala ijumaa kila Siku n weekend na kila siku ni siku ya kazi
Alaf kuna ishu mtu akipata mali jamaa wanaweza wakakuua ni kweli?
 
Alaf kuna ishu mtu akipata mali jamaa wanaweza wakakuua ni kweli?
Hapana ,inategemea kuna ujambazi kuna kuibiwa kwamba hujui madini, kuna kupigana hasa shimo likitema ,mwenye nguvu ndo anachukua mzigo .swala la kuuliwa eti umepat mali hilo m sijawahi liona myb mahali pengine
 
Kuna mzigo unaitwa 'kuvuta felo', ukifika kwa mara ya kwanza hapo hujui dhahabu, wala haujui ponchi, cha kwanza lazma uanze na felo. ...!!! Mgongo na kiuno. ..uneza usizae tena!
[emoji1] [emoji1] [emoji2] ile hendo ya kuvutia fero ikichomoka huwa inapiga kifua hadi unazimia
 
Ilikuwa sehemu ya maisha yangu, machimbo niliyopitia ya kwanza kabisa yalikuwa yale ya yaliyoitwa ya Bariadi (Bulyanhulu),wachimbaji wa kabila la Wanantuzu waliyaita Bariadi japo yalikuwa wilaya ya Kahama. Siku hiyo niliambiwa tushuke kwenye "longobesi" shimoni kwa sharti la tukitoka tusiende kula papuchi hadi tutakapoupata mwamba wa dhahabu!! Nusra demu wangu anihisi nishakwaa kaswende. 1996 rafiki yangu Hamisi Mguga wa kijiji cha Kafita akiwa anakimbilia kuokoa mifuko ya mawe ya dhahabu alifukiwa na Magreda kwa amri ya mkuu wa nchi ili kumpisha mwekezaji ambaye kwa sasa anaitwa Barrick. Kakola kama mwekezaji huyo asingepewa ingekuwa mji mkubwa kama Kahama maana machimbo hayo yaliitwa nickname kama "Mama Huruma " maana yake huwezi kushinda njaa kwa wingi wa dhahabu uliokuwepo. Ni kipindi hicho nilikuwa siogopi mtu yeyote nikiwa na baba mdogo. Ni kipindi shule niliiona kama ujinga flani hivi Kumbe................
 
Kuna mzigo unaitwa 'kuvuta felo', ukifika kwa mara ya kwanza hapo hujui dhahabu, wala haujui ponchi, cha kwanza lazma uanze na felo. ...!!! Mgongo na kiuno. ..uneza usizae tena!
Wavuta felo hata chakula chao ni mlima (hasa makande). Kwa kifupi ukizoea maisha ya machimbo ni sawa na kuwa teja.
 
Wavuta felo hata chakula chao ni mlima (hasa makande). Kwa kifupi ukizoea maisha ya machimbo ni sawa na kuwa teja.
Bila kusahau mboga ni dagaaa daily. [emoji3] [emoji3] nakumbuka tulikuwa na claim holder mmoja, dagaaa zikiisha ataenda chuma majani ya mmea wowote eti ndio mboga. .!! Majani ya mbigili, migunga, matunduru, majani ya chochote kile..!! HUYO SITAKAA NIMSAHAU.
 
Kuna siku jamaa walinikaribisha chakula, nikanawa nilipomega tonge nikakumbana na mboga ya ukwaju. (ukwaju umelowekwa kwenye maji kupata mchuzi).
 
Kuna siku jamaa walinikaribisha chakula, nikanawa nilipomega tonge nikakumbana na mboga ya ukwaju. (ukwaju umelowekwa kwenye maji kupata mchuzi).
Mboga inatiwa chumvi ya kutosha na Pili Pili ya kufa jamaa. ....!!! Hapo ugali utaisha mboga itabaki na ya jioni.
 
Tuliwah kuloweka dagaa wiki nzima dagaa zinabaki tunachemsha mchuzi kupata harufu ya dagaa ,ugaliwa mlima
 
Back
Top Bottom