Wale tuliomaliza Pepa za CPA leo tujipe pole

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
Wadau,

Wale tuliogonga pepa za NBAA leo, poleni sana. Maana kitu cha MA kilisimama sana, na wale wa Module E naona IF ilikua ndefu mno.

Masaa matatu yasingetosha kumaliza yale maswali yote ya IF na zile maksi moja moja zao za kichoyo. Otherwise tusubir end of December!!
 
Nendeni "mkagandishane" hadi matokeo! On a serious note: kila la heri mkuu!
 
TUNAWATAKIA KILA LA HERI MLIOFANYA MITIHANI HIYO YA CpA MUNGU ATAWASAIDIA MTAFANYA VIZURI
 
Naweza kusoma cpa uku nachukua degree

CPA ina stage kama tatu hivi, lakin ya mwisho ni "FINAL STAGE" ambayo ina phase mbili, Module E na F. Sasa ili uweze kufanya hii phase (final) inatakiwa uwe na moja kati ya Advanced Diploma ya Account, Degree ya Account au Finance na Module D ambayo wanaitoa wenyewe NBAA.

Kukujibu swali lako ni kua kwanza inategemea unataka kufanya level gani, kama ni final itawezekana tu kama tayari una level ya Module D.
 
Nasikia ukiwa na CPA wewe unalipwa si chini ya milioni ni kweli?
 
Jaman procedures za kusoma acca, hasa kwa mimi ambaye niko mbali tuisheni centers na benefits zake kwa mtu aliyejiajiri
 
Poleni sana.Msikate tamaa ,mtapata tu CPA na hongera pia kwa kufanya mtihani kuna wengine wanaingia mitini kwa woga.😛ray2:
 
Maelekezo mazuri sana ila hapo kwenye degree ya finance hawaruhusiwi kuingia module e ,wanaanzia module b...
 
Nimepitia paper ya Auditing sijui wale ambao hawa practice Audit watafaulu vipi! Alafu Contemporary Issues wameua kabisaaa! nina uhakika Qn no. 5 hakuna aliyegusa mnabisha? Hata mimi ningerudishwa sichomoki aiseee!
 
Tar 6 December 2012 ukumbi wa AICC Arusha on Accountants Annual Conference wanatoa rasmi Silabasi mpya na kwa tetesi zilizopo Final Stage itakuwa na masomo 10,unapiga 6 alafu unamalizia 4 ukimaliza hapo kutakuwa na paper ya mwisho inaitwa INTERGRATION OF KNOWLEDGE!

Piganeni msikutane na hii kitu mupya aiseee!
 
Nasikia ukiwa na CPA wewe unalipwa si chini ya milioni ni kweli?

Ndivyo inavyotakiwa kua mkuu, but utakua affected na vitu kama experience, labda kama umefanya sana kazi ukarudi kusoma cpa

Ila kama pengine umeunganisha direct from chuo una njaa kidogo so hata 1mil unachukua tu huku ukitafuta experience.
 
final kwaiyo mpaka nimalize bachelor

Hapana. Unaweza kumaliza CPA yako hata kabla ya kumaliza bachelor. Na haijalishi unafanya bachelor ya nini...as long as umekubali kuanzia mitihani ya level ya chini ya Bodi,,kama atec I,II etc na una speed ya kutosha ya kufaulu mitihani kwenye single sittings
 
Nimepitia paper ya Auditing sijui wale ambao hawa practice Audit watafaulu vipi! Alafu Contemporary Issues wameua kabisaaa! nina uhakika Qn no. 5 hakuna aliyegusa mnabisha? Hata mimi ningerudishwa sichomoki aiseee!

Watu tunabadilikia humo humo,,,kama vinyonga au Wenger akishauza Captain wake mwanzo wa msimu...as long as kuna wanaofaulu mwisho wa siku..haya mengine stori tu,,watu wameshangaa sana MA pia,walitaka maswali ya direct ya computations...,ha ha
 
Ile Auditing hata kama ungeruhusiwa kuingia na madesa bado ngoma ingekuwa nzito! Pale ni experience tu na si kukariri definitions!
 
Nasikia ukiwa na CPA wewe unalipwa si chini ya milioni ni kweli?

Raha ya CPA uwe na experience pia mkuu,utabadili kazi hadi uchoke mwenyewe alafu kote dau linapanda ila kama ndio wale from chuo then wanakomaa na CPA bila kufanya kazi lazima wakubali kuwa wadogo kwanza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…