Wale tuliosema Guardiola atafeli EPL tukutane hapa

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Wakuu habari ya leo!
Nawaomba wale tuliombeza Kocha bora kwasasa ulimwenguni kutoka Man City, Pep Guardiola kuwa atachemsha vibaya ndani ya ligi ngumu ya EPL tukutane hapa.

Baada ya mechi 11 za EPL, Pep Guardiola yupo kileleni kwa tofauti ya Point 8 dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili.

Pep anapata matokeo katika mechi zake, anapata magoli ya kutosha na pia timu yake inatandaza soka la kuvutia yaani kwakifupi anakufunga bila kubahatisha. Najua ni mapema sana ila nyota njema inaonekana asubuhi!

Wale wote ambao tulimbeza Guardiola njooni hapa tukutane, tutoe ushuhuda!
 
Ligi huisha may sio November hii au December, kwa hali ilivyosasa Chelsea, Manchester united na Tottenham wote wana nafasi kubwa tuu.
Tusubiri mpaka February hivi akiendelea na moto huu basi tumpatie tuu ubingwa mapema.
Ila jinsi navyoijua EPL Kuna mida ya xmass pale Kuna kuwa na shuguli pevu, mancity anfield pale pia hatotoka na point hata moja kwa speed walonayo Liverpool pia Kuna vitimu kam Burnley siku ukienda kwao wanakuamulia tuu kukutoa jasho.
Nadhani uliangalia mechi ya manCity na westbromiwich wikiendi ile iliyopita walishinda ndio ila kwa tabu tabu Jana pia bila maamuzi flani ya kisenge ya referee labda arsenal wangepata nguvu.
 
Ligi bado mbichi, hizi tathimini na tambo walau uanze kuzitoa kuanzia xmass
 
TEAM MBOVU KAMA MAN U INAFUNGWA NA [HASHTAG]#HUDDERSFIELD[/HASHTAG]
 
Ngoja tuone mpaka x-mass ndo tunaweza kutoa hitimisho
 
Mimi mmojawapo, ingawa ni mapema ila tukubali tu, Pep ni kocha bora duniani. Ni zaidi ya Mourinho maana anakupa na burudani ya mpira, tik tak. Namtakia mema achukue vikombe kuthibitisha hili.
 
X mass atakua anaongoza ila kombe hachukui
 
Pep kwa rasilimali alizo nazo (pesa + quality players) sioni kama msimu huu kuna team inaweza kushindana nae pale EPL

Ila huwa nashindwa ku judge ujuzi wa kocha na aina ya wachezaji alionao.

Mfano, tukimpa Pep team kama Arsenal hivi anaweza kwa wachezaji wale wale kufanya anayofanya akiwa na Man City?

Kiujumla simkubali sana kocha anafundisha team iliyojaa ma star kibao wanaojua mpira. Kocha anapata sifa kutokana na matajiri wa club kuvunja benki na kumkusanyia mashine za kazi. Wanamrahisishia kazi. Kama Zizzou sijahawi kumkubali kiivo kwamaana amekuta team ya watu wanaojua, angalia saivi wamechoka nae kocha anaanza kuwa exposed, anaonekana hajui. Time will tell.


Anyways mpira siku hizi umebadilika sana, kama haupo tayari kuvunja kibubu na kununua wachezaji wanaojua kwa bei kubwa basi ujue utaishia kushiriki tu na gombea kumaliza top four.

Wenye pesa za mafuta ndio watashinda Ligi kila msimu.

Tupambane na hali zetu jamani.
 
Mimi mmojawapo, ingawa ni mapema ila tukubali tu, Pep ni kocha bora duniani. Ni zaidi ya Mourinho maana anakupa na burudani ya mpira, tik tak. Namtakia mema achukue vikombe kuthibitisha hili.
jana nimekubali kweli pep ni professor wa soka, zile pasi za maudhi walizokuwa wanagongewa arsenal ndani ya box, nikajua kweli jamaa anaujua mpira wa kitabuni kuliko wenger, mana arsenal huwa wanajiona wao ndio wapiga pasi epl
 
jana nimekubali kweli pep ni professor wa soka, zile pasi za maudhi walizokuwa wanagongewa arsenal ndani ya box, nikajua kweli jamaa anaujua mpira wa kitabuni kuliko wenger, mana arsenal huwa wanajiona wao ndio wapiga pasi epl


Exactly mkuu!!! Pep ni fundi bwana. Na ufundi wake kaupatia kwa mchezaji wake wa zamani/King Messi.

Inshort bila ya Messi pep angelikuwa wa kawaida sanaa. Mkuu ukiangalia hata tik tack mwanzilishi ni Messi.
 

Hivyo ndivyo bingwa anavyopatikana, mechi inakuwa ngumu unashinda kwa tabu au kwa kupendelewa.
 
United kila mwaka utasikia kombe letu. mwisho wa msimu hewa tu.
- Wachezaji wa United ukimuondoa Herrera, Rashid, Masho na DeGea ndio wenye mpira . Wengine wanatumia nguvu nyingi bila akili.
Man United hawezi beba EPL 2017/18
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…