Oh, nafurahi kuwa ulipona na tatizo lako la fungus…japo nimekuta umepona, nakupa pole kwa mateso yaliyokupata!
tatizo ulilokuwa nalo ni kweli kabisa ni fungus, nilipokuwa sekondari niliwaji kupata na iilisababishwa na kuvaa chupi bila ya kujifuta maji mara baada ya kuoga au kujitawaza! Pia kurudia kuvaa chupi bila kufua…kwa kifupi ni uchafu na unyevunyevu ndio haswa ndio visababishi vya kuwafanya kuvu (fungus) hao kuota na kukua.
dalili ni hizohizo kujikuna sana hata kujichubua ngozi na kusababisha majeraha ambayo hutoa majimaji na baadaye kuweka tabaka gumu ambalo pia huwasha sana. Ukioga maji ya baridi utapata maumivu siyo ya dunia hii na hivyo unashauriwa kuoga maji ya vuguvugu! Mara unapooga zingatia kujifuta vizuri na upake antifungal powder na siyo dawa yoyote ya cream au majimaji. lengo ni kutengeneza mazingira makavu ktk maeneo ya sehemu za siri. na kumbuka kupiga pasi taulo ili kuua kuvu wanaojishikisha kwenye taulo. Pia ukumbuke kuvaa chupi safi na kamwe usurudie kuvaa chupi chafu.
Dawa kama mycota powder ni kiboko kwa aina ya kuvu hawa na ukianza kuitumia matokea ni ndani ya masaa 24 hali inadarikia na unapomaliza wk unakuwa na dalili za kupona kabisa. Lakini hata hivyo unapaswa uendelee na matibabu kwa takribani wiki mbili baada ya dalili zote kupotea.
Niseme tena pole sana kwa maswahibu yaliyokukuta na samahani kwa kuwa sikutembelea janvini kwa kipindi kirufu sana.
enzi hizo mimi niliubatiza ugonjwa huo wa fungus kama 'pumbu erosion' yaani 'mmomonyoko wa korodani/mapumbu!