Wale tuliosoma Makongo Secondary School tukutane hapa

Wale tuliosoma Makongo Secondary School tukutane hapa

Aisee Senkondo ndio yule jamaa wa misosi au...?. Huyu Afande Master nilimuacha na nyota 2 alikuwa mrembo lakini akikutia mkononi babake, hatari.

Kuna jamaa alikuwa anaitwa Issac tulikuwa nae bweni mshkaji alikuwa DAH acha nisiseme tu mtakuwa mmeshaelewa walengwa.

Ilikuwa ukipelekwa 1MP aisee ukirudi unaambiwa kabisa kapumzike bwenini usiingie class maana kipondo utakachopata pale acha tu.

Namkumbuka Salama Jabir na FILA yake aisee.
Safi sana Mkuu na ww kumbe tuko pamoja chama la Makongo duuuuuu.
 
Kuna Mtoto wangu alikuwa anatafuna Bazoka ( Big G) alipomuona Askari aliekuwa anawasimamia akiitwa Afande Miraji aliamua kuitema, Yule Afande alimlazimisha aiokote aitie mdomoni then aimeze, Mtoto nae Kwa hofu akatekeleza amri ile ya Kikatili!

Aisee Asubuhi niliamkia Kwa Kanali Kipungu nae ndio wale wale akaona Ni sahihi ile adhabu

Nilimhamisha Shule

Watoto wengi waliishia kuvuta bhangi Au Kuwa Watoro Na wengine wakawa ma Nunda

Makongo ya Miaka ya Mwisho ya 1990 lilikuwa Genge la Wahuni Kama Jitegemee
Teh teh teh Mkuu Makongo ya miaka hiyo ilikua moto sana aise maana nidhamu na matokea yake yalikua mazuri sana kuliko sasahivi imebaki jina tu.
 
Kwa wale tuliopitia Makongo kuanzia enzi zabkuvaa kaptura mpaka suruali tukutane hapa kama wahenga tukumbushane ya kihenga kuanzia makundi ya NO LIMIT SOLDIERS, FEHAJ SISTERS....

Bila ya kuwasahau maafande wetu Mzee Kipingu, Marehemu Mzee Yeyeye, Mzee Miraji, Babu Chacha na wengineo na kwa wale waliofariki Mwenyezi Mungu azilaze roho mahala pema pepon.

Kulikuwa na vitu kama NYAMBIZI, majuto garden na kwa wale wenzangu wa bweni hawatawasahau akina MASTER MAYEBE, MSONGOLE, MATAULA, SENKONDO, ANKO PETER na wengineo

Tiririkeni wahenga wenzangu
We utakua intake moja nami au intake zilofata.sie ndiyo tuliizindua nyambizi mwaka 2000 necta.

Hiyo majuto habari ingine..
 
Huyo afande atakuwa alikuwa Kapteni kisarika

Huyu jamaa ndio mkono wake wa kulia kama umepinda flani hivi right...?

Dah, jamaa anachapa kama ndio huyo aisee. Halaf alikuwa sio mtu wa kuongea ila ukiingia kwenye 18 zake ni shida aisee.
 
Wakati wa Assembly hupenda kusema

"Order of Matching, No change.."
 
Kuna Mtoto wangu alikuwa anatafuna Bazoka ( Big G) alipomuona Askari aliekuwa anawasimamia akiitwa Afande Miraji aliamua kuitema, Yule Afande alimlazimisha aiokote aitie mdomoni then aimeze, Mtoto nae Kwa hofu akatekeleza amri ile ya Kikatili!

Aisee Asubuhi niliamkia Kwa Kanali Kipungu nae ndio wale wale akaona Ni sahihi ile adhabu

Nilimhamisha Shule

Watoto wengi waliishia kuvuta bhangi Au Kuwa Watoro Na wengine wakawa ma Nunda

Makongo ya Miaka ya Mwisho ya 1990 lilikuwa Genge la Wahuni Kama Jitegemee
Siyo kweli mie nimemaliza F4 1994 kulikuwa hakunA hata nafasi ya kuvuta bangi na tulikuwa tunajisomea shule ya msingi makurumula,acha uongo toto lako miaka hiyo lilikuwa vutaji toka nyumbani kwako,Makongo hukuweza kuilinganisha na Jitegemee kwa nidhamu miaka ile
 
Makongo enzi hizo ilikuwa kituo cha taaluma, sanaa na michezo...akina Marehemu Chifupa, Daz Nundaz, Bon Crewz akina Eazy Mchwampaka, Salama Jabir, Mishi Bomba, Irene Ngowi nk kwenye kikapu sasa akina Gwantwa, Mpoki, Salum Kaindu, Kapwapwa, Mwaipungu, Gunze, Mlekwa, Jacob nk ilikuwa kwere kisanga na nususu
 
Back
Top Bottom