Siku zinakimbia kwa kasi sana wakuu, leo nimeamka natoka kwangu ile kufungua geti nakutana na mwalimu wangu mjeda wa Makongo yeye ameshanisahau kabisa ananunua kiwanja kinachopakana na Mimi, baada ya kusalimiana na kubadilishana namba nimemuacha aendelee na ratiba zake.
Nikaanza kukumbuka matukio yaliyokuwa yanafanywa na hawa walimu wajeda pamoja na wanafunzi enzi ninasoma pale shuleni na ikizingatia moja ya kigezo kilichofanya nipelekwe pale ni utukutu uliopitiliza.
Ukiachana na matukio mengi yanayonihusu nikiwa mwanafunzi pale nitaelezea mawili tu kabla ya wasomaji waliosoma pale nao kutoa vioja walivyoshuhudia wakiwa pale.
Binafsi nilikuwa mchelewaji sugu pale shuleni kutokana na muda mwingi kuutumia kupiga mapindi mchikichini, kwa mliopita pale mnaelewa ugumu wa mchelewaji kipindi hicho kupita pale getini Sasa ma-MP na karibia walimu wote wakawa wameshanijua.
Siku hiyo tumechelewa na group langu tumetoka mchikini tumekula chabo pale getini MP wako busy wanaongea na raia yaani tulipita pale Kama mshale ila mwenzetu mmoja akadakwa, kuchungulia Darasani pia kuna mwalimu wa Additional Mathematics mnonko kwelikweli na yeye, ikabidi twende nyambizi tukasolve vitini vya mchikini ili kipindi chake kiishe tuingie Darasani.
Tukiwa tunasolve vitini pale Nyambizi, mara akatokea mwanafunzi wa kike shombeshombe zuri kweli akakaa kimbweta pale karibu na Nyambizi hall, zoezi la kusolve vitini likaisha mjadala ukahamia kwa yule mdada.
Jamaa wakaanza, wewe Paploman ni mpori pori sana demu viwango vile huwawezi kabisa na kweli kipindi hicho muoga sana kutongoza pamoja na utukutu wangu wote nilikuwa na kula vya kunyonga tu, mjadala ukawa mkali yule dada kumbe alikuwa anasikia akawa anatabasamu tu, vijamaa vikaanza haya nenda Sasa mtoto kashakuelewa nenda kachombeze, nikajikuta mpole shinikizo lilivozidi nikaona isiwe shida nikajitoa ufahamu.
Nikamfuata yule dada alipokaa, huku vijamaa vinashangilia kufika pale nikamsalimia mdada akaitikia, nikamnong'oneza " Wale jamaa wananinanga eti sijui kutongoza watoto wazuri Kama wewe, Sasa naomba nikukumbatie usichukie ili niwaoneshe naweza"😄 demu akacheka akanipa go ahead. Nikamkumbatia na kumpiga bonge la busu vijamaa vikalipuka bonge la shangwe kumbe mwalimu wa zamu Kombaa (huyu alikuwa anafundisha French) na Master wametuona na wameona lile tukio wakiwa maeneo ya kantini.
Wakatufuata Mimi Sina habari niko busy na demu kumbe wenzangu washawaona wamekimbia kimyakimya, kuja kushtuka hawa hapa hata nguvu ya kuamka nikawa sina nikakamatwa kama kuku na vile huyu master vipindi vyake nilikuwa siingii nikaanza kula stiki palepele na kurukishwa kichura mpaka ofisi ya KIPINGU.
Kufika kule sikupewa hata nafasi ya kujieleza, stiki zikatembea tena za kufa mtu sasa Kombaa akaanza kumueleza KIPINGU alichonikuta nafanya akawa anasema "KIONGOZI huyu hili ni onyo la mwisho kwake, akirudia tena ni kufukuza shule kama utakataa basi niko radhi unifukuze Mimi"
Sasa kimbembe kingine nikawa nimevaa fulana ndani ya shati la shule na sheria za pale zilikuwa haziruhusu, nikaambiwa kuvua ile bado najishauri maana ofisini kulikuwa na walimu wengi nikala mvua za stiki tena kuja kushtuka niko kifua wazi, Master ananiambia "Kifua chenyewe kimejaa manyoya, wewe utakuwa chimpazee kabisa😃😃" mbele ya walimu.
Msaga sumu (R.I.P) alikuwa peace sana ila mimi hatukuendana na alifanya nikachukia kabisa practical za chemistry mwanzomwanzo baadae alinipa ushauri na tukawa karibu na nikamzoea.
Huyu Master ndio kabisa zikawa haziivi, Kuna siku darasani aliwahi kunipiga na mbao ( zile ruler kubwa za kupigia mistari ubaoni) kisa nimempa swali gumu la maths na nikaonesha kupinga njia aliyotumia na jibu alilopata akaona Kama namfanyia dhihaka swali nalijua, akanitolea maneno makali sana mbele ya darasa " Wewe utafaulu form4 lakini kwa mwenendo ulio nao form six PCM huwezi kufaulu, nitakufatilia nione" nilimjibu mwalimu lazma nipate One na maths na physics lazma niwe na "A" na kweli ikawa hivo matokeo yalipotoka, na yeye ndio alisababisha sikutamani kusoma advance japo nilichaguliwa ilibidi nibadili nikaenda DIT.
Enzi hizo kulikuwa na sheria za kijinga pale shuleni yaani huruhusiwi kupanda daladala kituo cha hapo shule, mjeda kabisa anakaa anaangalia atakaepandia hapo anashushwa na anapewa adhabu ilikuwa ni kupiga mguu hadi mwenge, makonda walikuwa wanasurubiwa sana pale enzi hizo.
Pamoja na utukutu wa wanafunzi wa pale kipindi Cha nyuma bado walikuwa wanafanya vizuri sana katika nyanja zote elimu, michezo, music, utangazaji na mengineyo.
Makongo ya Sasa sio O'level Wala Advance imeporomoka utafikiri sio Makongo iliyokuwepo zamani.
Karibu marijendari wa Makongo tukubushane mititi tuliyopitia pale shule.