Christopher Wallace
JF-Expert Member
- Dec 8, 2015
- 1,479
- 3,788
Wiki chache zilizopita mawakala wa DStv walitushawishi tujiunge na Dstv business kwa kifurushi cha Work Essential ambacho tulikuwa tunalipa 28,000/= na kupata mechi za EPL, La Liga, Serie A, Europa League na mechi chache za Uefa Champions League.
Sasa kumbe ulikuwa mtego, watu tukaunganishwa kwa wingi kwa kigezo cha kutuma namba ya dikoda, namba ya simu na tin namba na wengineo walidaiwa hadi leseni ya biashara.
Hatimae tukaungwa tukaanza kula burudani kwa elfu 28 ndio elfu 28 tu.
Kifurushi kikaisha muda wake bhana, kuunga tena inagoma? Ikabidi niwapandie hewani DStv, wakaniambia kifurushi cha elfu 28 hakipo, hivyo unatakiwa ulipie kifurushi cha elfu 81 kile wanakiita Work Ultra.
Nikawaambia siwezi, basi niondoeni kwenye DStv business ili nijiunge na vifurushi vya kawaida wanasema kwasasa hawana hiyo huduma.
Naamini sipo peke yangu, kama umekutana na hiyo kadhia karibu jukwaani tufarijiane...