Wale tuliounganishwa na kifurushi cha DStv Business halafu wakatubadilikia tukutane hapa tujifariji

Dstv hakuna haja ya kuwapigia unabadilisha mwenyewe
 
Hata dstv mbona wanafanya hvyo huna haja ya kuwapigia unafanya mwenyewe kupitia app ya dst au ussd code unatop up then unapandisha kwenda kifurushi unachotaka
 
Utapeli mkubwa daah poleni wakuu
Kiuhalisia sio utapeli, bei ya vifurushi vya dstv kwenye sehemu kama bar, kazini n.k ni tofauti na bei ya dstv kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Nadhani walitumia ujanja kuwanasa.
Kuna kipindi walikuwa wanawatumia vijana wanapita na kifaa fulani kama remote kwenye mabaa wakiclick kama king'amuzi hakijasajiliwa kutumika kwenye baa wanaona na wanaona namba za king'amuzi wanapeleka ofisini wanakifunga. Walikuwa wanapewa comission kutokana na ving'amuzi walivyonasa nadhani tshs 10000 kwa kila king'amuzi
 
Dada mwajuma kila siku nakuambia uwe unatumia kichwa kufikiria badala ya masaburi, kitonga gani wakati tulikuwa tunalipa pesa zetu
Kama ulikuwa na uwezo wa kulipia mwanzo lipa na sasa au umeachwa na mumeo aliyekuwa anakulipia?
Imagine mwanaume mzima na kende juu unakuja kulalamika kupandishwa kwa bei ya package ya DSTV? Unatakaje kwa mfano?
Kila kitu kimepanda bei hata bei ya unga wa dona iko juu tofauti na Januari/Februari nk.

Maisha yakikushinda tafuta mume msaidiane.
 
Dstv zilivyo kama nyanya saivi kila kona wana lilia wateja kwa bei kitonga, kumbe wana jua wata rudisha pesa yao chapu tu...
 
Duhh.. sio poa hii wazee.. huu mbona ni ujambazi live!!
 
Sitaki hata kuwasikia Azam. Wamewafanikiwa kuwasikia wanawake tu na watoto kwenye tamthilia za Revenge hata haiekeweki. Ukija kwenye Etigul na Ottoman nazo ni ovyo ovyo tu kila siku mapigano yasiyoeleweka yanakoanzia. Mtu anakuwa adui yako bila sababu. Wanawake ndio tamthilia zao. Nafikiri Wanaogopa kulipia tamthilia nzuri za kizungu. Kwenye tamthilia nimerudi zangu ITV,hawayumbi,tangu enzi za ACAPLUCOBAY na CAMILA. Matamthilia yao sio ya maigizo igizo,ni Yale ya serious

Ukija kwenye mpira wanaonyesha Ujerumani na ufaransa. Wameingia mitini kuonyesha ligi pendwa kama Uingereza na La Liga na Ligi ya mabingwa. Wameboa sana
 
Biashara ya dstv hua ipo kwenye kucheza na akili ya mteja. Wakikuona unawashobokea sana lazima wakuchezeshe

Mimi hua nafanya hivi....

Nina dstv na azam. Dstv hua sijiungi zaidi ya miezi 3 mfululizo...hivyo hua wakitaka kunizoea waanze kunichezesha ghafula sipo hewani (nimehamia Azam)...matokeo yake wanaanza kunipigia na kunitumia msg za promosheni kibao wanabembeleza nitumie kifurushi chao. Nikijiunga tu simalizie miez 3 lazima mwezi mmoja niwapitishe kapa
 
wahi wateja wako riverside wanaisubiria tgo yao
 
Sasa hivi ni rahisi kushtukiwa kwakuww dikoda ya biashara lazma iwe na nembo ya glass upande wa kulia wa tv yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…