Wale tuliwahi kupigana na walimu/mwalimu shuleni tukutane hapa

Unaonekana ulikuwa huna adabu halafu kaongo balaa.Na huyo mjomba wako hakuwa na busara na ujana ulimsumbua.Leo hii ukimkumbusha mlichomfanyia mwalimu wako atakulaumu sana.VIPI,siku hizi umekua?
kweli mkuu unayoyasema kuniadhibu alikuwa sawa sababu nilichelewa!
Lakini yeye alizidisha kipimo.
Naomba alipo popote namuomba anisamehe sana! Sio yeye tuu walimu woote pl/sec mnisamehe sana
 
Lemme tell you something! Nilipokuwa darasa la saba nilikuwa natandikwa sana viboko na mwalimu mmoja wa hisabati kwa kutofikisha alama alizonipangia.Miaka hiyo kulikuwa na warudiaji sana wa darasa la saba(wale ambao hawakufaulu ).Kwa kuwa kabla ya hapo nilikuwa ndiyo kidume darasani kwa kuongoza,walipofika nilirudi nyuma kimaendeleo ya masomo.Nakumbuka walikuwa takribani 12.Kumbuka hapo ni miaka takribani 30 nyuma. Basi,mwalimu wa hisabati alitupangia kwa makundi Alana za kupata.Kulikuwa na waliopaswa kupata 20%,35%50%,70%,80% na 85%!Nikawa kwenye 85%Mimi nikawa mara ya kwanza naishia kwenye 70%Aisee,nilipigika kama mara nne hivi(majaribio manner mfululizo) Nilikaa nikatafakari.Kila ninapokwama kufikisha alama zitakiwazo na ninachuana na warudiaji moyo uliniuma sana.Nilikaza misuli.Warudiaji walinikoma na mwalimu yule alinipenda sana.Nilikuwa navuka hadi 90+% Mwanzo nilimchukia sana mwalimu na warudiaji wake lakini mwishowe nilimshukuru sana kwa kuninyoosha.Niligundua nilikuwa na changamoto zifuatazo;
-kuwaogopa warudiaji nikidhani wana akili kunizidi kumbe ni wajinga tu ndiyo maana walifeli.
-kuwachukia walimu waliowakubali warudiaji hao.Kumbe ilikuwa ni sehemu ya changamoto ya maisha nao walihitaji kusaidiwa/second chance.
-nilikuwa bado nina homa kali (hangover) ya kupokwa uongozi wa darasa kitaaluma nikanyong'onyea.Kumbe juhudi na maarifa na kuviruka vihunzi vya bakora vilinisawazisha nikaurudia "utukufu" wangu na ufalme kitaaluma.
-Hasira zangu kwa kutandikwa viboko vya kushindanishwa na warudiaji nilizitumia positively nikaweza.
MWISHO.
Sikumkunjia mwalimu ngumi.Nikayaona matunda.Nikajua kwamba "Life is a challenge, I had to meet it"! And,I smoothly did that!Hooray to me!
 
Dah...darasa la kwanza wiki ya 3...Kuna mwalimu wa kuchora alinizingua...nikamfuata ofisini..nikasambaratisha walimu ofisi nzima...na shule ikafungwa[emoji41]
 
Mimi ugomvi ulikua unasababishwa na mademu kwani kila wakijaribu kujiopolea wanakuta tayari nimeshaweka makazi kitambo....basi uhasama wa hapa na palee
 
kweli mkuu unayoyasema kuniadhibu alikuwa sawa sababu nilichelewa!
Lakini yeye alizidisha kipimo.
Naomba alipo popote namuomba anisamehe sana! Sio yeye tuu walimu woote pl/sec mnisamehe sana
Bravo! Ni mambo ambayo tunapaswa kuwaelekeza watoto wetu uvumilivu.
 
Clap for your damn self!

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Dah...darasa la kwanza wiki ya 3...Kuna mwalimu wa kuchora alinizingua...nikamfuata ofisini..nikasambaratisha walimu ofisi nzima...na shule ikafungwa[emoji41]
Hii ndoto unayoota, usiposhituliwa mapema utakojoa kitandani.
 
Utapata laana wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…