Wale tuliwahi kupigana na walimu/mwalimu shuleni tukutane hapa

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Uzima upo wakuu??

Uzi huu ni wa kushea experience yako ulipokuwa shule hasa ugomvi na walimu au wanafunzi wenzako.
Binafsi Mimi shule ya msingi mwalimu mmoja alikuwa wa hisabati.yeye nilimkutaga kwenye pagale (jengo ambalo halijamaliziwa) yupo na madam wanatongozana!
So nikatega sikio baada ya hapo nikacheka kwa nguvu! Wao ndani wakaniona,me nikakimbia!
Kesho yake sasa nimechelewa shule halafu yule ticha alikuwa ana zamu! Yaani alinigonga fimbo vibaya mno! Me nikamsukumiza kwenye kalo la maji akatumbukia humo! Mimi nduki mpaka home nikamkuta mjomba wangu, yeye alikuwa polisi, nikamwambia tukaenda shule
Tulipofika ofisini tukakuta yule mwalimu kalowana ndo ametoka kwenye kalo!
Nikamwambia mjomba huyu ticha huyu ndo alinichapa!
Mjomba alimbeba yule mwalimu mpaka nje, akamdumbukiza tena kwenye kalo!

Toka siku hiyo nilikuwa sichapwi kizembe. Ukizingatia mwalimu mkuu alikuwa ni best friend na mzee wangu!

Shea nawe Mwana jf historia yako
Pia ntaelezea kisa changu nilipokuwa sec
 
[emoji23][emoji23][emoji23] siku namaliza shule la saba kuna mwalim alikuwa mnoko sana anaitwa alitukimbiza kwenye mashamba ya shule, akaanguka kwenye mtaro akadondokea kidevu[emoji23][emoji23]
 
Write your reply...nilimcheka ticha alikuwa anafundisha hisabati darasani maana akati anaandika ubaoni chaki ilidondoka akainama kuiokota hapohapo aliachia ushuzi nlishindwa kuvumilia ndugu mtoa Mada japo wenzangu walijiziba midomo akaniona baadae akaamua kuniita ofsini akanizabua

sikukubali kpindi nlkuwa mtoto wa kitaa nina ndugu yangu anavuta bangi basi Yule ndugu yangu nilimwambia akawaambia wahuni wake "haiwezekani ampige dogo muhun mmoja alisema,,, kunya anye yeye halafu analeta ukuda" basi wakiji organize walikuwa wanne tukamvizia barabaran usiku anatoka kwa kademu Kake sjui mke wake maana ni mdada tu alkuwa kamchumbia kijiji jiran alitoka kumuona alikuwa anaendesha taratibu baiskeli yake aina ya phonex tulikuwa tunaliita tetanus maana likukata bahat mbaya ni bora ukachome hio sindano limechakaa sio poa

basi alkuwa anaendesha taratibu uku akiimba nyimbo zake za ottu jazz band basi wahuni wakasimama mbele ya barabara akasimamisha baskeli akawaambia wahuni na kiswahili chake cha kisukuma "madogo token hapo barabarani nitawagongaga"

wahuni wakacheka hahaha oyaa "kayuka" unamuelewa huyu mshamba anachoongea jamaa akasema hajui kiswahili mm nimejificha nachungulia basi bwana wakamfuata wakamkwida wakampa kichapo balaa alilia sanaa nikafunga shati kininja na Mimi nikaenda mzibua mafimbo baada ya hapo wahun wakachukua raba zake za DH (dingi hanauwezo) na shati lake la kitenge wakumuacha amezima akujaa class wiki anauguza vidonda matakoni

ila raba zake alimuona ndugu yangu kavaa na akaenda ripot kituo cha kijijini broo alivyopigwa vitasa na polisi aliongea ukweli ilibidi migambo itumwe kutufuata popote tulipo si unajua lile ni kosa la ushambuliaj na wizi

hahaha nmekumbuka mbali mtoa mada
 
daaah ndugu ungemuonea huruma aisee 😂😂
 
Wakuu mm sina history, yakumtia ticha vitasa.

But niliwahi tu kuwa na bifu na ticha wa Geography, baada ya kumwambia darasan kuwa kama hajui kufundisha aseme.

Bifu likaanzia hapo,

Aliishiaga kunipiga fimbo 5 tu,
Kwa makosa mengine,
Na tulikua tunapigana jicho tu la hasira, kila mmoja anamkaushia mwenzie.

Alinichongea kwa mzee, baada ya mzee kuja school, kisa nimevaa modo.

Nikashona bwanga la pima juu chini kadilia, siku zikasonga, hadi kumaliza.
 
Walimu ni watu wa kuheshimiwa sana. kwani bila wao sisi tusingekuwa hapa tuna type pia. walimu ni nguzo muhimu maishani mwetu! Mwalimu ni mzazi wa pili.

Tatizo linakuja pale wanaposhindwa kuafuata ethics za kazi yao na badala yake kuruhusu hasira imuongoze! japo wanafunzi huwa wanasumbua kama sio kukasirisha.
Kwa yale yote niliyowafanyia walimu naomba mnisamehe huko mlipo!
 
Uzima upo wakuu??

Uzi huu ni wa kushea experience yako ulipokuwa shule hasa ugomvi na walimu au wanafunzi wenzako.
Binafsi Mimi shule ya msingi mwalimu mmoja alikuwa wa hisabati.yeye nilimkutaga kwenye pagale (jengo ambalo halijamaliziwa) yupo na madam wanatongozana!
So nikatega sikio baada ya hapo nikacheka kwa nguvu! Wao ndani wakaniona,me nikakimbia!
Kesho yake sasa nimechelewa shule halafu yule ticha alikuwa ana zamu! Yaani alinigonga fimbo vibaya mno! Me nikamsukumiza kwenye kalo la maji akatumbukia humo! Mimi nduki mpaka home nikamkuta mjomba wangu, yeye alikuwa polisi, nikamwambia tukaenda shule
Tulipofika ofisini tukakuta yule mwalimu kalowana ndo ametoka kwenye kalo!
Nikamwambia mjomba huyu ticha huyu ndo alinichapa!
Mjomba alimbeba yule mwalimu mpaka nje, akamdumbukiza tena kwenye kalo!

Toka siku hiyo nilikuwa sichapwi kizembe. Ukizingatia mwalimu mkuu alikuwa ni best friend na mzee wangu!

Shea nawe Mwana jf historia yako
Pia ntaelezea kisa changu nilipokuwa sec
Ningekuwa mm mwalimu ningekutoa.utumbo
 
Unaonekana ulikuwa huna adabu halafu kaongo balaa.Na huyo mjomba wako hakuwa na busara na ujana ulimsumbua.Leo hii ukimkumbusha mlichomfanyia mwalimu wako atakulaumu sana.VIPI,siku hizi umekua?
 
[emoji48]
Ujinga Kugombana na Mwalimu , mkufunzi wako au mtu yeyote anaekuongoza ni kitu kibaya Sana kwani anaeza kufitinisha kwa namna yoyote ile ukashindwa kufikia malengo yako.
Success goes together with the Discipline.
 
Back
Top Bottom