Wale tunaoanza Ujenzi 2022, Tupeane Start up Dondoo

Kama uko serious huna mke, njoo inbox Nina mtoto wangu naimani atakufaa sana kama ataridhia lkn.
 
Hiyo kama ikikamilika kwa viwango na muonekano wake, gharama ni zaidi ya 250m, vinginevyo ataachia libak pagale!
 
Kha yaani wanatumia foood colour ndio wanakwambia treated....watu wa aya jamani
 
Ofcourse upo sawa baada ya kuwapa.wakadiria majenzi na wataalumu wa tadhimin wengi walichezea 80-100m but mm nimejipa kiasi cha chini ili niwe makini kubana matumizi but Kisaikologia najua itafika 100m..
Hiyo nyumba yako itakugharimu128 hadi 145 ukiweka ukuta itafika 168...na nje landscaping ni 183....ukiisimamia vizuri structure itakula 76m.servises weka 10m finishing weka 40m

Pambana....upambane maliza.....
 
Ukishakuwa na plot tu anza jenga mdogo mdogo utashangaa umemaliza tu
Haswaaa na hii ndo watu wengi wanatumia.Namwomba Mungu nifanikishe nipate plot kubwaaaa ili soon nikiipata nianze mwaga mawe na mchanga taratibu
 
Hiyo nyumba yako itakugharimu128 hadi 145 ukiweka ukuta itafika 168...na nje landscaping ni 183....ukiisimamia vizuri structure itakula 76m.servises weka 10m finishing weka 40m

Pambana....upambane maliza.....
Dah. yaan aisee mimi akili imekaa kwenye 100, ila ntapambana mpaka itakapo fikia .

Ila mkumbuke hii nyumba sehemu kubwa ni ya kawaida. hapo katikati tu ndio pana chumba cha kisasa Delux Master so hapo juu pana 5x6m beams 6 tu.. nangazi.. Naamini Designer alivyo idesign aliofanya ionekane Gorofa kwa kuweka hayo manguzo marefu ya mbele ya nyumba ila sehemu kubwa haina gharama ni msingi ya kawaida na corse za ukuta za kawaida .

Nilitak designer aifanye iwe na muonekano wa hadhi kwakuweka hako kagorofa juu ila isiwatishe ni wataalamu wa5 tofauti wameipitia hii raman na kila mtu ametoa makadiro ya gharama kitaalamu nawameangalia ulaji wa nondo na slab na kaeneo kanacho simamisha hicho chumba cha juu hivyo wameridhika haitatumia material mengi ..
 
Hongera sana mkuu, kwa maoni na ushauri tupo hapa kukusaidia
 
Uzi huu utakua kama ule wa kuichangia Simba uwanja.
Watu walikua wanatoa bilioni bilioni.
 
Kujenga nyumba ni uoga wa maisha.[emoji276]
 
Nimeambiwa ni kati ya 74_80milion
Lengo la aliyekupa makadirio ni zuri sana. Ametaka kuona umeanza kujenga.
Makadirio ya hiyo kitu kuisha haiwezekani ikawa hivo mkuu.

Ukianza hutoacha, huo ndiyo uzuri wake.

Na kingine, kama ungeweza kubeba material ikawa site itakupunguzia gharama za usafirishaji wa mara kwa mara, maana yake uweke store ya muda.

Usimamizi wako ni kitu muhimu sana tena sana.

All the best in your safari mkuu.
 
Usiogope juu ya mifuko mkuu. Inawezekana kabisa ikafika kulingana na eneo lako. Mifuko 300 mpaka 350 kwa eneo lako ni very possible.

Hilo lisikukwamishe. Fikisha mifuko 300 site then uwe na bajeti ya ziada siku ya umwagaji. Kwa maana siku ya kazi ikitumika mifuko nusu utakuwa umepata picha ya sehemu iliyobakia na kujua kama unapaswa kuongeza mifuko au iliyopo inatosheleza.

Ukifuata vinavyoandikwa na mafundi unaweza usijenge maisha.
 
Anzisheni uzi wenu muweke kazi zenu tutawasapoti
 
MKO VIZURI HONGERENI MNAOJENGA, WENGINE NGOJA TUPANGE TU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…