Wale tunaoanza Ujenzi 2022, Tupeane Start up Dondoo

Wale tunaoanza Ujenzi 2022, Tupeane Start up Dondoo

Wanasema asiye kujua akikuona barabarani anakujaji kwa muonekano wako.. ila natamani ungejua maish niliyo kulia nahata sasa una weza niona nina kazania kitu ambacho labda wewe huna ila kumbe wewe una mengi ambayo mimi sina.. mafano hapo una gusia ada za januari wakati mimi naumri huu sina mtoto na sinafuraha kwenye eneo hilo na umri huu .. Kama una baraka ya watoto na mke wwngine hatuna natuna 33yrs ila hatuna mke wala mtoto na kwenye eneo hilo hakukai sawa kabisa kumeshindikana.. sasa nikuulize ikiwa una mtoto na mke uambiwe unipe mimi hiyo mke na mtoto alafu mimi nikuachie nyumba hii ninayo jenga utakubali?
Kama uko serious huna mke, njoo inbox Nina mtoto wangu naimani atakufaa sana kama ataridhia lkn.
 
boma tu itafika hio ila sio na finishing ile ya final
kitachokula hela kwanza msing wake.nondo zitaenda za maaana,halalf jamv lichekechwr na mashine listop wekk 3 zije nguzo nazo zisetiwe zimiminwe zivekwe majunia zimwagiwe angalau wek 3 aje slab la juu nalo sion hio 80 kama itatosha na huo mwez mmoja hautosh
Hiyo kama ikikamilika kwa viwango na muonekano wake, gharama ni zaidi ya 250m, vinginevyo ataachia libak pagale!
 
Mwenzetu wewe haupo kwenye mawazo ya tarehe 17 wala kodi...maisha ni vidole hayawezi kufanana...
😁😁😁 Mkuu wewe size yako ni kama hizi

IS-HAQ R. MPONDA.png


IS-HAQ R. MPONDA1.png


MWAMBESO FINAL PLAN.png


MWAMBESO FINAL PLAN1.png


MWAMBESO FINAL PLAN2.png


MWAMBESO FINAL PLAN3.png


MWAMBESO FINAL PLAN4.png


ASUKILE KALINGA FINAL NO.2.png


ASUKILE KALINGA FINAL NO.21.png


ASUKILE KALINGA FINAL NO.23.png
 
Kwanza hongera kwa udhubutu.
ILa kwa 80mil sidhani kama nyumba itaisha kwa ramani uliotupia umu pitia upya makadilio yako usije ishia njiani ukizingatia vifaa vingi vya ujenzi vimepanda ghalama.
Kuwa makini na nondo zipo famba mtaani ukitaka jua ilo chukua chache tengeneza umbo la U ikikatika achana nayo utakuja haribu nyumba.
Kuwa site mda wote mafundi wengi wapigaji anaweza taja ela ndogo kwa labour charge akijua atafidia kwenye kukwapua material.
Paa kwa ramani iyo ni vyema ukawa na option mbili
1.bati dizaini ya kigae
2.kazia kigae cha Nabaki Africa au ALAF warranty 50 years
Pia zingatia kutumia treated timber sio izi ambazo watu wanatreat na food color mtaani kuwa makini
All the best comrade.
Kha yaani wanatumia foood colour ndio wanakwambia treated....watu wa aya jamani
 
Ofcourse upo sawa baada ya kuwapa.wakadiria majenzi na wataalumu wa tadhimin wengi walichezea 80-100m but mm nimejipa kiasi cha chini ili niwe makini kubana matumizi but Kisaikologia najua itafika 100m..
Hiyo nyumba yako itakugharimu128 hadi 145 ukiweka ukuta itafika 168...na nje landscaping ni 183....ukiisimamia vizuri structure itakula 76m.servises weka 10m finishing weka 40m

Pambana....upambane maliza.....
 
Ukishakuwa na plot tu anza jenga mdogo mdogo utashangaa umemaliza tu
Haswaaa na hii ndo watu wengi wanatumia.Namwomba Mungu nifanikishe nipate plot kubwaaaa ili soon nikiipata nianze mwaga mawe na mchanga taratibu
 
Hiyo nyumba yako itakugharimu128 hadi 145 ukiweka ukuta itafika 168...na nje landscaping ni 183....ukiisimamia vizuri structure itakula 76m.servises weka 10m finishing weka 40m

Pambana....upambane maliza.....
Dah. yaan aisee mimi akili imekaa kwenye 100, ila ntapambana mpaka itakapo fikia .

Ila mkumbuke hii nyumba sehemu kubwa ni ya kawaida. hapo katikati tu ndio pana chumba cha kisasa Delux Master so hapo juu pana 5x6m beams 6 tu.. nangazi.. Naamini Designer alivyo idesign aliofanya ionekane Gorofa kwa kuweka hayo manguzo marefu ya mbele ya nyumba ila sehemu kubwa haina gharama ni msingi ya kawaida na corse za ukuta za kawaida .

Nilitak designer aifanye iwe na muonekano wa hadhi kwakuweka hako kagorofa juu ila isiwatishe ni wataalamu wa5 tofauti wameipitia hii raman na kila mtu ametoa makadiro ya gharama kitaalamu nawameangalia ulaji wa nondo na slab na kaeneo kanacho simamisha hicho chumba cha juu hivyo wameridhika haitatumia material mengi ..
 
Hongera sana mkuu, kwa maoni na ushauri tupo hapa kukusaidia
 
Mimi nimeanza leo kwa kupita kwa wauza matofali, Nimechagua tofali zangu 5000 fundi wangu akazikagua ubora nikalipia.

Tukapitia Kwa wauza Kokoto JKT nimelipia Lori 2 nyeusi.

Nimepewa number za wasambazaji wa Mchanga nime agiza lori 4.

Nimepita Duka la Hardware nime nunua Nondo za 16mm pc 25.

Jioni hii nimepita Kwa wauza Cement nime lipia mifuko 50 ila itakuwa inaletwa site taratibu kwa itaji la siku la Mafundi maana hawako mbali na site yangu na sina pakuweka.

Kwa sasa Niko mahali na Taka kununua Tank la Majin la simTank la l lita 4000lt.

Siku yangu imeisha kwa-ubize huu...

Vipi wenzangu!?? Mliopanga kuanza ujenzi mwaka huu mna mikakati ya kuanzaje.. ??

Pia naomba Wajenzi wazoefu nishauri chochote hapo.

Site yangu ipo Mbezi Beach ya Salasala Mwisho wa Lami mita 200 tu kutoka Lami ilipo.

Vifaa ni vyakuanzia tu awamu ya kwanza.. Nyumba niliyo ipost hapa chini ndio Ninayo ijenga na hiyo ni moja ya Mchoro wa Actual drawing from Wachoraji.View attachment 2065228View attachment 2065227
Uzi huu utakua kama ule wa kuichangia Simba uwanja.
Watu walikua wanatoa bilioni bilioni.
 
Nimeambiwa ni kati ya 74_80milion
Lengo la aliyekupa makadirio ni zuri sana. Ametaka kuona umeanza kujenga.
Makadirio ya hiyo kitu kuisha haiwezekani ikawa hivo mkuu.

Ukianza hutoacha, huo ndiyo uzuri wake.

Na kingine, kama ungeweza kubeba material ikawa site itakupunguzia gharama za usafirishaji wa mara kwa mara, maana yake uweke store ya muda.

Usimamizi wako ni kitu muhimu sana tena sana.

All the best in your safari mkuu.
 
Nahisi mwenzangu Huna stress mimi ni ujenzi wa kwanza ramani yangu na yako hazitofautiani ila kuna pahala nime doubt fundi anasema foundation nitahitaji mifuko 400 eneo langu sio slope ni hapa shule ya msingi Ali hapi karibu na Moga primary school naomba nipe uzoefu mwenzangu foundation fundi kasema mifuko mingapi...maana mimi ukubwa wa jengo ni mita 21 kwa 21. Tafadhali nahisi anataka kunipiga...material zote nimeshakusanya kama wewe kasoro sementi nasita nahisi hakuna uhalisia...Tafadhali share uzoefu.
Usiogope juu ya mifuko mkuu. Inawezekana kabisa ikafika kulingana na eneo lako. Mifuko 300 mpaka 350 kwa eneo lako ni very possible.

Hilo lisikukwamishe. Fikisha mifuko 300 site then uwe na bajeti ya ziada siku ya umwagaji. Kwa maana siku ya kazi ikitumika mifuko nusu utakuwa umepata picha ya sehemu iliyobakia na kujua kama unapaswa kuongeza mifuko au iliyopo inatosheleza.

Ukifuata vinavyoandikwa na mafundi unaweza usijenge maisha.
 
Oraa tupeanage na connection wengine humu mafundi wazuri tuu, mtupege madili, sio kututangazia mambo yenu na plan zenu wakat mnatunyima madili...

Mafundi wote humu em tuzame DM kwa huyu mleta mada akatuambie vzr tareh husika ya sisi kuanza kaz[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Anzisheni uzi wenu muweke kazi zenu tutawasapoti
 
MKO VIZURI HONGERENI MNAOJENGA, WENGINE NGOJA TUPANGE TU
 
Back
Top Bottom