Wale tunaopenda vacation, sehemu gani ya utalii Tanzania uliyofika au unatamani kufika?

Wale tunaopenda vacation, sehemu gani ya utalii Tanzania uliyofika au unatamani kufika?

Kuna maeneo kadhaa mazuri ya kutembelea mkoani Mbeya, jumlisha na mkoa wa Songwe
  1. Kawetire view point - Njia ya kwenda Chunya. Pale utaona bonde la ufa kwa ukubwa wake, yaani ile trough (beseni) la bonde la ufa, ni sehemu nzuri sana. Iko njia kuu ya kwenda Singida na Tabora eneo la Kawetire
  2. Daraja la Mungu, likpo Rungwe Mbeya. Ni mwamba mgumu (jiwe) ambao umevuka mto na pana mandhari nzuri sana ya kuvutia. Jirani na hapo pana kijungu (maji ya mto yanapotelea ardhini)
  3. Tembelea Matema, fukwe za ziwa Nyasa. Kuna fukwe nzuri sana na utapata nafasi ya kuogelea ziwani, maji baridi burudani kabisa na utapata nafasi ya kula samaki wa ziwa Nyasa
  4. Eneo la Songwe (Majimoto) kuna majimoto (geysers) yanayotoka ardhini. Maji ni ya moto kiasi unaweka yai linaiva na unakula. Kijiji kipo kilometa 8 kutoka uwanja wa Ndege wa Songwe, kama unaelekea Tunduma
  5. Ukipata nafasi temebelea kimondo cha Mbozi, eneo la Ndolezi, nao ni utalii tosha.
  6. Mwisho, tembele mbuga ya maua ya Kitulo, ni mwendo wa saa 2 kutoka Mbeya mjini, uelekeo wa Makete Njombe kupitia Igoma.
Thanks sana
 
Ila wadau vacation ni muhimu sana kuweka kichwa sawa.

Hata kama umepigika kiasi gani jitahidi kwenda vacation at mara moja kwa mwaka ukakae sehemu na familia hata siku mbili tatu. Inasaidia sana kutuliza kichwa na kuweka muunganiko wa familia.

Maisha mafupi haya tusiishie kuchangia harusi tu, tuweke na akiba kidogo kwenda vacation na familia hata mara moja kila mwaka. Kuna raha sana kukaa fukwe za bahari na familia zetu. Kubadilisha mazingira ya nyumbani na pia kula misosi tofauti na ya nyumbani.

Napenda vacation
Aisee Una Akili nyingi Sana mkuu
 
waandikie bei hiyo ambayo wewe wasema sio kubwa kiivyo waione
Self service bufee BF 45k
Bia 6.5k mtaani 4000/3000
Imported bia 9k.. ambazo mtaani ni 5k
Kitimoto 36k
Fish fillet 36k

Unless bei ziwe zimebadilikwa kwa mwaka huu.
 
Self service bufee BF 45k
Bia 6.5k mtaani 4000/3000
Imported bia 9k.. ambazo mtaani ni 5k
Kitimoto 36k
Fish fillet 36k

Unless bei ziwe zimebadilikwa kwa mwaka huu.
Mkuu mtaani bia 2000 Tsh. 🙌🏻🙌🏻😁
 
Habari zenu wadau, uzi huu ni maalum kwa ajili ya kucomment sehemu yoyote ile ya kitalii uliyokwishafika au unapenda/kutamani kufika kwa hapa Tanzania au nchi za jirani na Tanzania.

Karibu uweke comment yako.
Mbinga Hadi Nyasa mbambabay, hutojuta
 
Ntyuka Dodoma chini unaiona UDOM makazi mapya
20240116_101552.jpg
 
Maisha mafupi haya tusiishie kuchangia harusi tu, tuweke na akiba kidogo kwenda vacation na familia hata mara moja kila mwaka. Kuna raha sana kukaa fukwe za bahari na familia
Sisi wengine tunaishi Fukweni na Familia Mwaka hadi Mwaka
 
Back
Top Bottom