Wale tunaovaa Barakoa tupeane experience jinsi ya Kuvaa, mwenzenu inaniletea matatizo

Waziri wa Afya alikataza tusivae Barakoa namba N95 sababu ni chache na tuwaachie wahudumu wa afya. Kwakuwa hili swala linahusu uhai, imebidi nitafute hizi kwani nahisi zitakuwa na ubora zaidi.
View attachment 1431943
View attachment 1431952

Nafikiri hutakiwi kuvaa barakoa mda wote mkuu. Mfano kama upo ofisini peke yako, au uko kwenye sehemu ambayo haina mkusanyiko, unaweza kuvua. Barakoa inavaliwa kwenye yale maeneo hatarishi kama sokoni, madukani, kwenye usafiri wa umma nk. Pia aina ya barakoa unayovaa inachangia. Hizi N95 na jamii yake upumuaji unakua tabu kidogo japo ndio nzuri.
 
Halafu masikia yalivyoumbwa utadhani yalikuwa yanasubiri kuwekewa barakoa
 
Juzi kati nilikuwa nakula msosi nimeweka barakoa pembeni naendelea kula nikajisahau nikadhani tissue nikajifutia mikono. Hivi vibarakoa special vyeupe disposable. Roho iliniuma sana
 
Kichwa kinauma Kinyama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna drop lets zinaweza penya kwa chini ya barakoa labda kama ni za sayansi ya risasi iliomuua Aquilina (rejea maelezo ya afande) hivyo sio lazima ukaze hizo kamba hadi ukose hewa. Jaribu kulegeza kidogo mkuu. Pia vaa pale unapokuwa maeneo yenye msongamano tu. Sio hata kwenye gari uko mwenyewe unakomaa tu.
 
Mimi sasa

1. Kupumua kwa shida sana

2. Masikio yanauma kwa kutanuliwa na kamba za barakoa

3. Mpaka korona itakapoisha nitakuwa na masikio yamepanuka kama ya paka au kama ungo

Hivi watz nani aliyesema barakoa inavaliwa masikioni???
 
Hata mimi zinanipa shida sana,barakoa zinatakiwa kuvaliwa wakati wa dharura tu au unapotoka nyumbani,lakini ukiwa nyumbani sidhani kama ni lazima uvae muda wote,mimi nikivaa kwa saa moja tu nasikia mapigo ya moyo yanaenda kasi,pia macho yanawasha na hata pua inawasha,labda waliozoea hizo barokoa ni watu wa viwandani na waganga au wale wanaoishi nchi zenye uchafuzi wa mazingira, nikivaa napumua kama chatu aliyetoka kumeza swala,hawa walioleta huu ugonjwa wametukomoa, hapana pa kukimbilia au kukwepea
 
Mvuta sigara na barakoa ni kutesana tu
 
Wewe utakuwa unatumia barakoa ya chini ya kiwango au saizi za nyusi za kichina.

Badala yake tafuta "gas mask" kama zile za kujikinga na maambukizi ya silaha za kibaiolojia na kemikali.

Pengine una uso na kichwa nje ya viwango vinavyojulikana na wenzetu huko duniani,

jifunze kutengeneza yako kwa vipimo vyako mwenyewe (kama tailored suit) hapa...

 
Barakoa inasaidia kubana matumizi kwa wavuta sigara maana kama atavaa muda mwingi basi Atakuwa anavuta Ile harufu ya sigara inayotoka puani na mdomoni na hatimaye anakosa hamu ya kununua sigara mpya.
Mvuta sigara na barakoa ni kutesana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…