Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Huku kwetu Uswahilini choo kinatumika masaa 24 ya siku katika siku saba za Juma.
Huna haja ya kusubiri tank lijae, unamsubiri aliendani amalize na wewe unaingia. Kama utakutana na ajali aliyetoka si mlengaji mzuri wa shabaha ni siri yako, inabidi usafishe kwani atakae ingia baada ya wewe atajua ajali ilikuhusu wewe.
Choo cha jirani kikijaa tunamkaribisha jirani na wapangaji wake watano ambao mmoja ana watoto watano, mwingine saba, huyu aliyehamia juzi amekuja na wake wawili na watoto tisa. Hawa wawili wana watoto watatu kila mmoja.