Wale wacheza kamari CASSINO tukutane hapa

Wale wacheza kamari CASSINO tukutane hapa

Nautico

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2017
Posts
341
Reaction score
788
Kwenu wana bodi hili liwe jukwaa kwa wacheza roullete,slots,black jack n.k tupeane story.


Kimsingi mimi ni mhanga wa cassino na mchezo wangu mkuu ni roullete,hua nacheza cassino za hapa Dar,Arusha,Mwanza na Nairobi.

Katika maisha yangu ya kamari hii pesa kubwa niliowahi kupata kwa mkupuo ni milioni 27 kwa kianzio cha laki 1 na nikamalizia nyumba iliobaki nikanunua harrie tako la nyani.

Pia nishawahi kuliwa milioni 8 usiku 1

Kama haitoshi pesa zangu zinaishia kwenye uraibu huu hatari.


Roullete ni mchezo hatari ambao kila baada ya sekunde 33 unaliwa au unakula.


Katika pitapita zangu nishawahi kushudia mtu ameliwa milion 350 kwa siku 1

Pia nishawahi shudia mtu kaja kununua roli pesa ikaliwa cassino milioni 45.


Kama haitoshi kuna dada mmoja mfanyabiashara wa Tanzanite aliliwa milioni 84 akataka kuweka bond gari lake na alikua kwenye vikao vya ndoa yake hali iliopelekea kuahirisha ndoa juu ya kamari.


Kwa haya na mengineyo karibuni tujadili mstakabari wa hili janga.

Upande wangu naomba serikali ufutilie mbali aina hii ya michezo.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pesa kubwa niliyowahi kuliwa Ni million Saba


Oya nawazingua buana Mimi nitapatia wapi million Saba cassino yenyewe sijawahi hata kuingia
Mimi Ni mdau was betting ya kawaida tu
Screenshot_20181229-102404.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Every hand is a winner, and every hand is a looser but INTELIGENCE matters.

Gambling haitegemei BAHATI peke yake, lazima uwe na kichwa chepesi, mwizi, muongo, mhuni, tapeli na KIPAJI pia. Lazima ujue muda gani utupe, muda gani usubiri, muda gani ukimbie mbio nyingi sana.

Nikiwa na miaka 21, nliwahi kumchapa jamaa kwenye POKER Million 9, siku hio hio hakuridhika baada ya kunikuta kwenye POOL TABLE nambaka mtu wash. Akaomba COLLABO ili atleast arudishe hata nusu ya hela yake. Nikagoma kuweka hela nikaomba tuweke bet gari (Hela nlikua nategemea kulipia ada chuo UDSM mwaka wa kwanza, kama week moja iliopita nlipigwa hela ya ada yote pamoja na hela ya kujikimu **Mkopo wa chuo wote, sio wa BOARD**, halafu baada ya week moja tulikua na paper kukamilisha Course Work).

Nlikua nimeenda na mshikaji wangu wa chuo ana Mark II, (Ilikua mbovu kinoma, imepigwa pasi kisawasawa, na kila kona ilikua na milio kama mashine ya kukoboa na kusaga). Jamaa akaweka GX 110 mpya bila hata kuhakikisha gari nlioweka mimi hadhi yake. Yule rafiki yangu nliekua nae alikua kawaka tungi huku akishangilia navochuana kwenye pool table, bila kujua gari yake ndo nimeiweka rehani.

Advantage nliopata jamaa nliecheza nae, alikua anataka kucheza kwa kukamia kisawasawa, so mi nika relax kinoma. Aliishia kuchezea WASH tatu straight. Na gari akaacha. Tunatoka casino na rafiki yangu kila mtu na gari yake, nlivomwambia gari yake ndio nliweka rehani, kwanza hakuamini na pombe zilimruka huku akiambatana na kunishushia matusi ya mama kifurushi cha siku.

*** Ila kuna mapigo takatifu unaweza ukapigwa casino, mpaka ukasikia kiungulia cha roho au kizunguzungu. Ushauri wangu, gambling/cassino/betting hazifai kabisaaaa ni rafiki wa umasikini.

#Poker My Fav, kupimana akili na uwezo.[emoji53] [emoji18]
 
Back
Top Bottom