Wale wafuasi wa Gamondi hatuwataki kuwaona wakijipendekeza timu ikifanya vizuri kwenye mashindano

Wale wafuasi wa Gamondi hatuwataki kuwaona wakijipendekeza timu ikifanya vizuri kwenye mashindano

vibertz

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2022
Posts
2,474
Reaction score
4,726
Kuna watu wamekuwa wakijifanya wapenzi wa Gamondi utafikiri walikuwa wanamjua huyo Gamondi kabla ya Hersi kumleta Yanga. Yaani anajifanya kususa timu kisa tu uongozi kuachana na Gamondi na kuwatoa akili viongozi. Hawa watu wamfuate Gamondi huko anakoenda na wawe mashabiki wa hizo timu badala ya Yanga.

Mashabiki wa kukosoa kitu kabla hata kujipa muda kusubiri kuona matokeo ya viongozi kuleta kocha mpya umejipa au lah. Kila mtu anajigeuza mtabiri, huku mwingine anaombea eti kocha afeli ili uongozi ujifunze kufanya maamuzi ya busara, na kwenda uwanjani eti umesusa, sasa huyu shabiki ana tofauti gani na mchawi? Yaani ikitokea Yanga inafanya vizuri lazima nafsi itamuuma sana kwanini inafanya vizuri. Na huyu inaonekana alimpenda kocha bila sababu ya msingi na hakupenda timu.

Nifah na wengineo risiti zenu zipo, wote mliokuwa mmekosoa maamuzi ya kuondoka Gamondi sasa ole wenu timu ikifanya vizuri mlete shobo zenu, kwasasa mfuateni Gamondi, sisi mashabiki wa Yanga tunaendelea na ushabiki wetu wa timu.
 
Hata wao watasema siku YANGA ikifungwa msiungane nao kulaumu uamuzi wa Viongozi.
Kwani kuna timu isiyofungwa duniani? Mbona Gamondi alifungwa dhidi ya Ihefu na Azam msimu uliopita na hakufukuzwa?
 
Hichi ulichokiandika hapa Sisi tabora utd inatuhusu nini?
 
Muda karibia unatoa majibu, kasi imerudi, morali imerudi, soka la kuvutia inarejea. Kuna kundi kubwa sana walikuwa wanamtoa akili Hersi na kocha wake aliyemleta utafikiri walikuwa wanamjua huyo Gamondi.
 
Mimi ni mmoja kati ya watu wa mwanzo kabisa kuanzisha mjadala wa Gamondi kutimuliwa. Ila bado ni mapema sana kusherehekea mafanikio ya kocha mpya.

Nadhani tungeendelea kumpa kocha mpya muda na pia kumwombea heri katika safari yake ya kuifikisha Young Africans mbali zaidi.
 
Performance tu ya Kibwana Shomari ni jibu tosha kuwa Gamondi alikuwa ni mtu wa tabia ya aina gani. Mimi niliamini sana katika kile kilichofanywa na viongozi na pengine Gamondi angeendelea kubaki tungeona kushuka kwa ubora wa Yanga na sio kupanda
 
Hakuna kocha duniani, anaeweza kuwa fair kwa wachezaji wote, ukurasa wa gamond ushafungwa tugange yajayo.
 
Taratibu wanafiki wameanza kujipendekeza kwenye timu Yanga, wakati walimchafua sana Hersi alipofanya maamuzi magumu kuinusu Yanga. Mbali na hilo kocha wakamponda sana hapo mwanzoni kuwa hana uwezo. Ila saivi wanajifanya gusa achia twende kwao.
 
Back
Top Bottom