Thanks kaka Bora uhai kwa kunifumbua macho ila kuna staff mwenzangu aliacha akafanyiwa hivi cjui ilikuwa sahihi au la 300000÷30=10000÷8hrs=1250×1.5×12hrs×12 months=180000. Alafu siku za sikukuu kampigia hivi 1250×2×8hrs×14days per year=280000 je ni sahihi? Hivyo ndivyo naona watu wakiacha kazi wanakokotolewa.
labda kama muajiri wako alikuwa halipi masaa ya zaida na sikukuu wakati unafanya kazi ila kama alikuwa analipa sizani kama ni sahihi kulipa na kwa ukukotoaji wa masaa ya ziada pia upo hivi kwa uelewa wangu
Kila saa linalozidi baada ya mda wa kawaida kwa mujibu wa sheria ni angalau ya 1 1/2 yani moja na nusu ya mshahara wa siku mshara wa siku ni 10,000 kwa masaa 8 kila lisaa 1250 kwaiyo tukifwata sheria hapo ni
2083 kila lisaa la ziada na hii ni kwa siku za kawaida na jumamosi ila jumapili inatakiwa kuwa mara mbili ya
2083 yani
4166
kwa saa ni 1250 ila linapokuja swala la overtime haItakiwi tena kuwa 1250 ila itatakiwa 1 1/2 ya 1250 alafu ujumlishe sasa ndo utapata kujua kila lisaa la overtime linathamani kiasi gani
Sasa basi kwa kawaida overtime, jumamosi & jumapili na siku za sikuu hujumuishwa katika malipo ya mwezi na kila mwezi mfanyakazi hupewa salary slip ikionesha mchanganuo
Nawaza kichwani mwangu yafuatayo
Imekuaje masaa ya ziada mtu alipwe pale anapotaka kuacha kazi iwe kama sehemu ya haki zake
Je unarekodi ya kujua kila siku baada ya masaa 8 ulikuwa unafanya masaa mangapi ya ziada kipindi chote cha miaka 2
Je unarekodi ya kujua jumamosi baada ya ile nusu siku ulikuwa unafanya masaa mangapi kama masaa ya ziada kipindi chote cha miaka 2
Je unarekodi ya jumapili ngapi ulizowahi kufanya kazi kipindi chote cha miaka 2
Je unarekodi ya sikuu ngapi ulizowahi kuzifanya kipindi cha miaka 2
KUMBUKA: CHUKUA HATA HICHO ENDELEA NA MAMBO YAKO