Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 12,463
- 27,556
Wakuu kama mjuavyo nikienda mahali huwa napenda kuwajulisheni namna kulivyo. Bila shaka mnajua wazi mimi ni mdau wa kilimo na ufugaji (mdau haswa sio mbabaishaji)
Huko kwingine tupo tu kwa sababu tunaishi dunia ya watu wa aina zote but kila nikifungua jf muhimu niingie jukwaa la kilimo na ufugaji na hata kabla ya kulala muhimu niingie kuangalia kulikoni. Bahati mbaya serkali haina habri nasi.
Ukiniona jukwaa lingine nipo kwa sababu nipo.
kiini cha uzi huu.
Ni kwa wale wanapenda kufuga au biashara ya kuku aina ya kuchi og mdomo kasuku. Waende mpanda katavi kisha wilaya ya Tanganyika Kata kwenda mwese nenda mazima hadi kijiji kinaitwa KASILIPU au Shukia kwanza MANYONI ukifika hapo uliza wenyeji wa hivyo vijiji. Kuwa nahitaji kuku aina ya kuchi. Hata ukikaa hapo manyonyi wasukuma hasa wamama au mabinti utaona wanakuja kuuza pale senta japo unaweza pata kuchi chotara kama huwajui vizuri. Ukienda ndani ndani unakuta familia yote ina kuchi watupu yaani hadi una wahurumia wapo uchi maana hawana manyoya na mvua za huko basi tu ..japo wengine wanayo manyoya.
Mimi nilienda Kaya 2 ili kwenda kuwabaini kama kweli ni wenyewe na kweli ni wenyewe kabisa maana huwa nawafuga kwa ajiri ya kula tu nyumbani kwangu.
Naweza kuwa na jogoo ili tu nipate nyama mixer. Bahati mbaya sana simu haikuwa na chaji sikuweza kupiga picha maana nilikuwa porini.
Walisema hata mji wa kapanga wanapatikana bei ni kama kuku wengine tu maana hawajui soko lao li wapi.
Yaani hawavuki 30k!
Tafadhar mimi siwezi kufuga kuchi maana hawazaliani sana na miyeyusho tupu hivyo kama nilivyosema hapo juu siwezi kuwaacha wao kwa wao tu ati wapandane la hasha lazima niwamix tu.(Hamchelewi kusema wewe umenunua wangapi)
Hayo nimefikisha kwenu. Ni taarifa sahihi kwa 100%kw wale wamefika huko watakuwa mashahidi wa hili.
Ahsante