Sasa hivi kuna visingizio vingi sana vya eda ya raisi Samia baada ya kufiwa mume wake, watu wakidai inabidi tuelewe kwamba ana eda ya miezi minne na siku 10 kwa ajili ya kufiwa mume wake, hata kama yeye alikuwa mke mdogo. Sasa tuwekane sawa.
Kwanza ieleweke katiba yetu ya Tanzania haina dini, na hakuna mahali inasema tukiwa na raisi muislamu wa kike, akifiwa mume basi atafanya/hatafanya yafuatayo akiwa eda. Raisi Samia sio muislamu pekee ambaye anapatwa na msiba wa kufiwa mume. Wapo wanawake makazini wengi tu ambao huko kazini wakifiwa na mume hatujasikia wakisema mie sintafanya/nitafanya yafuatayo kwa sababu niko eda. Sasa uislamu wa raisi Samia ni tofauti na wanawake wengine wafanya kazi katika mashirika au taasisi za serikali?
Pia, kama suala la eda ya miezi miine na siku kumi ni la lazima sana, basi ijulikane wazi kwamba Raisi Samia amekabidhi maradaka kwa Makamu wa Raisi katika kipindi hiki cha eda yake, na taifa lifahamishwe hivyo,ili awe huru kufanya/kutofanya mambo fulani kwa mujibu wa kanuni za eda.
Na zaidi, wale wanaosema ameenda Zimbabwe kuhani msiba wa Chivayo kisiri kwa sababu ya eda, watuambie kama eda inaruhusu ukiuke taratibu zake fulani ili mradi unafanya mambo kisiri. Kama raisi hakutaka ijulikane ameenda Zimbabwe kwenye msiba wa Chivayo, eda isifanywe kisingizio. Au kama alihutubia mkutano wa Wabunge wa dunia Arusha kwa video kwa sababu ya eda isemwe wazi,maana dunia haituelewi kumekuwa na minong'ono kuhusu hilo.
Na mwisho ningependa kuwauliza enyi waislamu. Kanuni ya eda, nini hasa lengo lake? Je, si kumfanyia heshima mume aliekufa kwa mjane wake kutoonekana hadharani na kujisahau labda kwa kuonyesha furaha na vicheko wakati wa kuomboleza, au kuji-expose hata kutongozwa na wanaume wengine wakati muda wa kuomboleza mume wake haujapita wa kutosha? Sasa kuna wasiwasi wowote kwa Raisi Samia kwamba haya yanaweza kumtokea? Vitu vingine twapaswa kuelewa badala ya kukariri kama kasuku.